GET /api/v0.1/hansard/entries/1073038/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1073038,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073038/?format=api",
"text_counter": 212,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sakaja",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13131,
"legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
"slug": "johnson-arthur-sakaja"
},
"content": "Jambo la tatu ni la kijografia. Ukiangalia mambo ya kijografia, alisema kwamba ni Mwenyezi Mungu ambaye aliamua sisi tuwe majirani na sio sisi. Tuko na mipaka baharini na ardhini katika nchi kavu. Ikolojia yetu ni moja. Alitoa mfano ambao Sen. Cheruiyot alijaribu kusema, kwamba, wanyama wetu wa pori hutoka Serengeti na kupata mimba katika Maasai Mara na wakirudi, hao ambao wamezaliwa tunasema ni wa Tanzania au Kenya? Kwa hivyo, kutokana na ukweli huo na ushirikiano kati ya Tanzana na Kenya, hatuna hiari, bali kufanya kazi pamoja. Mungu ameamua na sio lazima tuendelee. Katika uwekezaji, aliorodhesha Kenya kama nchi ya tano ambayo imeweka uwekezaji mkubwa sana nchini Tanzania na idadi ya takwimu ya Tanzania ambayo iliorodhesha. Ukiangalia Amerikani, Uingereza, kisha China na India, tuko na taifa la Kenya. Alisema kuna kampuni ya wawekezaji 513 kutoka Kenya ambao wanafanya biashara katika nchi ya Tanzania na wao wana kampuni kama 30 hivi ya kazi na biashara. Kuna Wakenya 2,000 ambao wameajiriwa katika nchi ya Tanzania na pia hapa tuko na Watanzania. Kwa hivyo, ni uhusiano ambao lazima uendelee. Nilifurahia sana vile aliweza kuwaonya wale ambao wanafanya kazi katika Serikali ambao hujaribu kuzingatia yale ambayo tunatofautiana kuzidi vile wanazingatia yale ambayo tunakubaliana. Ni jambo ambalo kwa Kimombo tunasema political goodwill . Kwa Kiswahili ni nia nzuri ya kisiasa ambayo inahitajika kati ya nchi zetu. Sio tu nia nzuri ambayo inapatikana katika Serikali upande wa utekelezaji au Executive, lakini pia uhusiano wa Mabunge yetu ni muhimu. Alitoa salamu kutoka kwa Spika wa Bunge la Tanzania. Bi Spika wa Muda, Rais wa Tanzania alimtaja Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alisema ya kwamba: - “Tukipoteza muda mwingi kuwagawana kibaba, tutapoteza wasaa wa kuvuna pishi.” Bi Spika wa Muda, nilikuwa na fursa ya kumtembelea Mama Maria Nyerere kule Tanzania. Nilipata fursa hiyo miaka miwili iliyopita tukiwa pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga na viongozi wengine. Tulikuwa tumeenda mambo ya michezo. Wakati huo alikuwa patron wa team ya Gor Mahia na mimi wakati huo nilikuwa pia patron wa team ya AFC Leopards. Huko Tanzania tulikuwa tumeenda kucheza na Yanga na Simba. Tulipata muda wa kuenda kumtembelea Mama Maria Nyerere. Hapo pia tulikutana na aliyekuwa Jaji Mkuu Warioba na viongozi wengine ambao wamekuwepo kwa muda mrefu. Nilifurahia kusikia wakisimulia uhusiano kati ya Kenya na Tanzania. Ukisoma kitabu cha aliyekuwa kiongozi shupavu Kenya, Bw. Tom Mboya, kitabu ambacho kinaitwa: “A Man Kenya Wanted to Forget” anasimulia vile alipokuwa anawindwa na wale wakoloni alipokuwa akiishi Shauri Moyo na Kaloleni hapa Nairobi. Walikuwa wakija kwa nyumba yake mara kwa mara na wanampata amekaa na Julius Nyerere wakizungumza mambo ya vile tutapata uhuru kati ya Kenya na Tanzania. Uhusiano wetu unaenda miaka na miaka. Ni vizuri ya kwamba tumepata kiongozi sasa katika Jamhuri ya Tanzania ambaye pia anataka kuhakikisha kwamba uwiiano na umoja huu utaweza kuendelea."
}