GET /api/v0.1/hansard/entries/1073040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1073040,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073040/?format=api",
    "text_counter": 214,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sakaja",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13131,
        "legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
        "slug": "johnson-arthur-sakaja"
    },
    "content": "Ningependa kuwasihi viongozi wenzangu tuzidi kutembeleana. Nilifurahi vile Rais Samia Suluhu alisema haitakuwa mara yake ya mwisho kuja Kenya. Tunamkaribisha aje tena. Ningependa kumwambia ya kwamba amekaribishwa Nairobi City County na akija wakati mwingine tutaenda kutembea na tuone sehemu nyingi katika taifa letu. Nina marafiki wengi katika Bunge la Tanzania. Ndugu yangu January Makamba ambaye aliwania urais alikuwa namba tano. Alikuwa na miaka arobaini. Nilimweleza, kweli mmepata rais mzuri. Alicheka na kusema, kweli tuko na rais mzuri. Labda miaka ijayo yeye pia atakuwa rais wa Tanzania. Huwezi kujua mipango ya Mungu. Labda mimi nitakuwa rais wa Kenya katika siku za usoni. Popote ambapo tutakuwa, tutahakikisha ya kwamba uhusiano wetu lazima uendelee. Nikimalizia ningependa kukubali ya kwamba kwa muda mrefu mimi mwenyewe pia nilikuwa miongoni ya wale ambao tulikuwa hatukubali kwa kina mambo ya political federation kati ya Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi. Lakini nakumbuka mwaka wa 2010 nilipokuwa na ambaye alikuwa Waziri wa Fedha wakati huo na sasa ni Rais wa Kenya alinikosoa akasema “hapana Sakaja”. Nilikuwa nafikiria kama uchumi wetu uko mbele, tukiungana na hizi nchi zingine uchumi wetu utashuka. Akaniambia “Hapana. Hapa Kenya tuko na shida ya ukabila. Tunafikiria kuhusu, Wakikuyu, Wajaluo, Wakamba. Sasa tukiongeza Waganda na Watanzania; nchi ambazo hawazingatii kabila, tutakuwa tumemaliza mambo ya ukabila. Ndio tunaweza kuwa labda tumepunguza vit i katika muungano wa mataifa lakini ile nguvu ambayo tutakuwa nayo kama political federation itakuwa nzuri zaidi.” Alinibadilisha mawazo kutoka siku hiyo na ninamshukuru sana Rais wetu wa Kenya kwa sababu alinibadilisha mawazo. Kwa sababu ya hiyo, ningependa kuhimiza wabunge mara nyingi tukifanya ziara, tunaenda kwa nchi za mbali, Marekani, China. Tutembee, Burundi, Tanzania na Uganda tuanze kujuana. Hii ni kwa sababu hizi nchi kubwa ambazo tunafanya nazo biashara ni Uganda na Tanzania, usare wetu pia itabidi iongezeke. Rais wa Tanzania aligusia miundo msingi, zile projects ambazo zinafanyika kati ya Kenya na Tanzania. Nitagusia tu kidogo kwa sababu ziko na manufaa mengi, sana kwa wale ambao wako Pwani na Sen. Madzayo atakubaliana na mimi. Ukiangalia barabara kutoka Lamu, Mombasa, Tanga, Bagamoyo ni kilomita 454. Hii itabadilisha uchumi. Rais wa Kenya alisema ya kwamba Watanzania wana uhuru wa kuja Kenya kufanya kazi bila kutafuta leseni ya kazi au work permit. Ningependa pia Bunge la Tanzania lijadili jambo hili pia watupe ruhusa wafanyibiashara wa Kenya wafanya vivyo hivyo. Aliongea juu ya barabara ya Arusha-Holili-Taveta-Voi ambayo ina urefu wa kilomita 2060 ambapo pia huko niko na ukoo kidogo. Huko tuko na mambo mengi ambayo yanafanana kuliko hata ukoo. Barabara hiyo itasaidia uchumi na watu wetu wataweza kusafiri kufanya biashara baina yao. Ilifunguliwa rasmi mwaka wa 2012. Pia, kuna mambo ya huduma za mipakani ama one-stop border post. Hiyo one- stop border post hapo Namanga na Holili, Taveta, vituo hivyo vimeahirisha shughuli za"
}