GET /api/v0.1/hansard/entries/1073042/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1073042,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073042/?format=api",
"text_counter": 216,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sakaja",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13131,
"legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
"slug": "johnson-arthur-sakaja"
},
"content": "biashara mipakani na uvukaji wa watu. Kuna mambo mengi ambayo tunaweza kufanya kati yetu. Tunamshkuru sana kwa kuja hapa na ninaomba kwa sababu alimwalika Rais wetu Uhuru Kenyatta awe mgeni wa heshima katika wakati watakuwa wanaadhimisha siku yao ya uhuru, ningeomba pia apewe heshima vile, pia aweze kuhutubia Bunge lao kwa sababu mambo ambayo atatamka hapo, itabidi mawaziri wetu wahakikishe yametekelezwa. Naomba ya kwamba kusiwe na yeyote katika Serikali yetu ambaye atakataa kufuata amri ambayo Rais wetu alisema na kusiwe na yeyote katika Serikali ya Tanzania ambaye atatenda kinyume na maagizo ambayo Rais Suluhu alisema. Mwisho kabisa alisema ya kwamba tumeanza ushirikiano wa kupigana na mambo ya COVID-19. Nimefurahi vile alikuja, tuliona alikuwa amevaa barakoa. Juzi amepata ripoti kutoka Wizara ya Afya, aliuliza wale ambao wamekimu katika mambo ya biolojia na kutoa ripoti ya kwamba sasa wanafuata sayansi. Tunawaombea kila la kheri Watanzania. Ningependa waje Kenya wazungumze na KEMRI kwa sababu KEMRI wamepata uzoefu wa mambo ya testing ya COVID-19 na kupata chanjo ya COVID-19. Tunawaombea kila la kheri. Tunaomba pia wafuate masharti kwa sababu hatungependa kupoteza ndugu zetu Watanzania kwa janga hili la COVID-19. Tunamshukuru sana Rais Suluhu Hassan. Karibu tena Kenya; karibu tena Nairobi."
}