GET /api/v0.1/hansard/entries/1073043/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1073043,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073043/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bi Naibu Spika wa Muda, kama ingekuwa mtihani wa Kiswahili, nafikiria ndugu yangu Sakaja, ama wale wanaomuita “Saks” kama mimi, ningekuwa nimempatia asilimia 99 juu ya mia moja. Ameongea Kiswahili sanifu ambacho kimeeleweka katika kuchangia katika huo mjadala wa kuhusikana na Mhe. Suluhu, Rais wa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania, ilikuwa jambo la kutabasamu. Ninafurahi sana na ningependa kumhimiza, aendelee na moyo huo huo. Endelea na Kiswahili hicho hicho na nina hakika kila mtu katika Kenya leo amekuskia ukiongea Kiswahili, tena sio kile Kiswahili cha sheng, ni Kiswahili mufti. Asante Bi. Spika wa Muda."
}