GET /api/v0.1/hansard/entries/1073061/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1073061,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073061/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cherargei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13217,
        "legal_name": "Cherarkey K Samson",
        "slug": "cherarkey-k-samson"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, ninatoa shukrani zangu kwa kunipa fursa hii niweze kuchangia hoja hii kwa siku ya leo. Mwanzo kabisa namshukuru Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mhe. Suluhu Hassan, kwa kufanya ziara rasmi nchini Kenya na katika Bunge la Kitaifa na Seneti. Nilikuwa na fursa nadra na adimu sana kuwa baadhi ya viongozi ambao walihudhuria na kusikiliza Hotuba ambayo alitoa katika Bunge la Kitaifa. Tulijua kwamba kiongozi wa awamu ya sita Mhe. Suluhu Hassan ni kiongozi ambaye ameleta undugu na urafiki hasa katika mataifa yetu mawili ya Tanzania na Kenya. Bi. Spika wa Muda, ningependa kugusia mambo matatu kulingana na hotuba yake. Kwanza ni kumshukuru na kumtakia kila la heri hasa wakati huu anapochukua hatamu za uongozi ingawa alichukua wakati ambao mtangulizi wake; Rais John Pombe Magufuli, aliaga dunia. Nilifurahishwa sana kwa sababu alitushangaza sana kusema kwamba anafuatilia hasa hoja na miswada ya mabunge mawili, hasa Bunge la Seneti. Huo ni wakati tulitoa risala zetu za rambirambi na pole ambazo ziliwekwa katika kumbukumbu la Bunge la Seneti. Hiyo ilikuwa inaonyesha kuwa tuko na uhusiano ama mnato fulani kati ya nchi hizi zetu za Kenya na Tanzania. Aligusia mambo mawili na kwanza ni kuhusiana na uwekezaji. Alisema kwamba mataifa ya Tanzania na Kenya yako na kurasa mpya ikizingatiwa mtangulize wake hayati Rais Pombe Magufuli alikuwa na kusisitiza kuwa Tanzania kwanza kuliko nchi nyinginezo. Nafikiri uwekezaji ambao tumepata kama taifa hili umetupatia changamoto, hasa wafanyibiashara wetu. Bi. Spika wa Muda, tumeona kwamba hata ingawa tulikuwa na wasiwasi kidogo wakati kulikuwa na mkutano katika hoteli ya kifahari hapa jijini Nairobi, kuna mfanyibiashara mmoja kutoka nchi ya Tanzania tuliona katika kanda ya video katika mitandao ya kijamii. Alikuwa analalamika kwamba ameshindwa karibu miaka miwili au tatu kupata fursa ya kufanya biashara katika taifa letu la Kenya. Nafikiri hiyo ni changamoto ambayo taasisi ambayo inahusika na uwekezaji ambayo ni Kenya Investments Authority (KIA) kushughulikia masuala hayo ndio tuweze kuwa na yale mambo ambayo tunatakikana kufanya biashara kwa njia rahisi. Tuhakikishe"
}