GET /api/v0.1/hansard/entries/1073063/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1073063,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073063/?format=api",
    "text_counter": 237,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cherargei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13217,
        "legal_name": "Cherarkey K Samson",
        "slug": "cherarkey-k-samson"
    },
    "content": "ofisi za Serikali zinasaidia wawekezaji wapate fursa ama wasisumbuliwe. Kama ni kupata stakabadhi ama leseni fulani ili waweze kufanya biashara basi wapewe nafasi hiyo. Hii ni kwa sababu hatuwezi kutegemea nchi za ng’ambo kama Uchina, Marekani na Uingereza. Lazima tuanze katika nchi za Afrika. Nafikiri ni muhimu kama tunaweza kufanya hivyo. Bi. Spika wa Muda, akaweza kutaja mamilioni. Inaonekana Wakenya wanafaidika zaidi hasa tunapoweza kufanya uwekezaji katika taifa la Tanzania. Nataka niwasihi kwa sababu hata alitoa changamoto kwamba wafanyibiashara wanachukua hatua muhimu zaidi kuliko serikali zetu. Nafikiri serikali, na alituomba kama Bunge la Taifa na Seneti, tuweke sheria ambazo zitasaidia kurahisisha na kuhakikisha kuwa biashara katika kanda hili la Afrika Mashariki imenufaika. Jambo la pili ni kuhusiana na mambo ya biashara. Dada yangu Sen. (Dr.) Musuruve amesema kwamba kulikuwa na tofauti, hasa wafanyibiashara ambao huwa wanachukua watalii kutoka Kenya au Tanzania wakija nchini Kenya. Alisema suluhu tutaweza kupata. Amesema yeye atakuwa suluhu kulingana na jina lake na kuhakikisha wale wafanyibiashara ambao wanasafirisha watalii wanaendelea na shughuli zao bila pingamizi yoyote. Bi. Spika wa Muda, pia tumeona wale madereva wa malori ambao wanasafirisha bidhaa kutoka nchi yetu wakienda katika Tanzania na wakitoka Tanzania wakija Kenya. Wamekuwa wanasumbuliwa kwa sababu ya kupimwa maradhi ya korona au COVID-19 na pia kuhusu mambo ya ushuru. Amesema ni muhimu Wakenya waelewe--- Ni kuwa Kenya na Tanzania wataweka huduma za pamoja mpakani ama kwa lugha ya kimombo,"
}