GET /api/v0.1/hansard/entries/1073065/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1073065,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073065/?format=api",
    "text_counter": 239,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cherargei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13217,
        "legal_name": "Cherarkey K Samson",
        "slug": "cherarkey-k-samson"
    },
    "content": "Ndio wahakikishe tuwe na utaratibu na tusiwe na msongamano wa magari ambao wanasafirisha bidhaa zao kutoka nchi ya Kenya kuelekea Tanzania ama kutoka Tanzania wakielekea Kenya. Hiyo ni muhimu. Alisema tutakuwa na huduma za pamoja mpakani. Ninamshukuru Rais Suluhu kwa sababu hiyo ndio imekuwa ikileta joto la kibiashara kati ya mataifa haya mawili. Bi. Spika wa Muda, tuko na ukanda wa pwani ama ile inaitwa coastal corridor. Ni muhimu kuhakikisha wale wanaoushughulika mpakani kama maafisa wa ushuru na uhamiaji wahakikishe wamefanya njia iwe rahisi. Jambo la tatu ni Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwanza, tuna Bunge la Afrika Masharika. Bunge la Seneti tuko na kamati maalum ya kushughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Bi. Spika wa Muda, hata wewe mwenyewe umewahi kuwa Mbunge katika Bunge la Afrika Mashariki. Tunawapa heko na kongole waheshimiwa Wabunge kwa sababu wamejaribu kuleta uhusiano mwema kati ya mataifa ya Afrika Mashariki. Tunataka kuona mng’ato katika kibiashara, undugu na jamii. Sio tu kijiografia lakini katika uwekezaji na biashara."
}