GET /api/v0.1/hansard/entries/1073069/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1073069,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073069/?format=api",
"text_counter": 243,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cherargei",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13217,
"legal_name": "Cherarkey K Samson",
"slug": "cherarkey-k-samson"
},
"content": "Viwanda vinahitaji umeme. Lazima tuwe na umeme wa kutosha. Kwa hivyo, ni lazima turekebishe sekta ya umeme katika taifa letu. Tumeongea na wawekezaji wengi sana katika taifa letu, na wengi wao wanalalamikia bei ghali ya umeme. Tukifanya ushirikiano kwa sekta ya umeme, itarahisisha kufanya biashara katika taifa letu. Hii itafanya tusipoteze wawekezaji kwa sababu ya bei ghali ya umeme. Bi. Spika wa Muda, mhe. Samia aligusia jambo la bomba la gesi litakalotoka Tanzania hadi Kenya. Ni jambo muhimu sana kwa sababu sheria ya swala la fedha za mwaka wa 2021/2022 imesema kwamba kutakuwa na kodi kwa mambo ya gesi. Tunajaribu kuwaambia Wakenya wasitumie kuni kupika chakula kwa sababu wanaharibu mazingira. Tukipata bomba la gesi nchini Kenya, wananchi walio kwenye vitongoji kama Kibra, Mlango Kubwa, Mathare na kadhalika, wataweza kupata gesi kwa bei nafuu. Tuchunge mazingira yetu na tuhakishie kuwa ni safi kwa sababu tutakuwa na bomba la gesi litakalofanya bei ya gesi kuwa nafuu. Nina mambo mawili mazito ya kumalizia nikikunja jamvi. Ningependa Seneti izingatie ushirikiano wa usalama, taasisi za Serikali, madola ya Serikali na mambo ya usalama. Hii ni kwa sababu tunajua kuwa kuna changamoto ya uhalifu, ugaidi, maharamia wa bahari, na ushirikiano wa taasisi za usalama. Pia, kuna mambo ya ufisadi. Tunataka kuona ushirikiano kati ya wale wa wanaopambana na rushwa katika Taifa la Tanzania na tume ya kupambana na ufisadi katika taifa letu. Wafanye ushirikiano ili wale wanaojaribu kuiba pesa za umma wasiweze kuziweka nchini Tanzania au Kenya bali wafunguliwe mashtaka. Ninafikiri kuwa hii ni muhimu. Bi. Spika wa Muda, ningependa kusisitiza kuwa tuwe na ushirikiano wa taasisi za usalama. Taasisi za kukusanya ushuru nchini Tanzania na Kenya wawe na ushirikiano, ili tuwapatie wafanyibiashara na wawekezaji nafasi bora ya kufanya biashara kwa urahisi. Hii itasaidia uchumi wetu kukua. La mwisho, kama vile Sen. Sakaja alisema, kazi ambayo Rais Suluhu Hassan--- Baada ya kutoka hapa, jopo hilo limeanza kupendezeka kuwa waanze kuvaa barakoa na kuzingatia sayansi kukabili Virusi vya korona. Nilifurahi wakati niliona Rais Suluhu Hassan akiwa kwenye mkutano wa wazee. Alitoa ilani kwa umma kuwa lazima wavae barakoa nchini Tanzania. Hii ni muhimu kwa sababu janga la korona limeendelea kuhangaisha watu kiafya na kiuchumi. Tumefurahi kwa sababu tumeona kuwa jopo hilo limesema kuwa wanaweka mipango kabambe kuhakikisha wamezuia kuenea kwa virusi vya korona katika taifa la Tanzania na Jumuia ya Afrika Mashariki. Tunapoongea, nchi ya India imekuwa na mlipuko wa jana wa korona. Ni lazima tuwe na mpango kabambe. Lazima Rais Suluhu Hassan ahakikishe kuwa wameingia katika muungano wa COVAX, kama walivyoambiwa na World Health Organization (WHO). Hii itahakikisha kuwa wamepata chanjo za Korona katika Taifa la Tanzania. Jambo ambalo wenzangu hawajagusia ni kuwa tumeona kuwa kulikuwa na msukosuko wa kisiasa. Nchi ya Tanzania walifanya uchaguzi mwaka jana. Tuliona Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Mapinduzi (CCM), ambacho kinaongozwa na Rais wa sasa."
}