GET /api/v0.1/hansard/entries/1073071/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1073071,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073071/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cherargei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13217,
        "legal_name": "Cherarkey K Samson",
        "slug": "cherarkey-k-samson"
    },
    "content": "Kulikuwa na kutoaminiana na ukiukaji wa haki za kibinadamu. Kuna watu waliokuwa wameshikwa kwa sababu ya siasa. Taarifa kwamba Rais Suluhu Hassan hakuwaachilia walioshikwa kwa sababu ya kupigania haki za binadamu na siasa haikudhibitishwa. Bila kuzingatia dini, chama au siasa, ningemuuliza Rais Suluhu Hassan ajaribu kuwaleta Watanzania pamoja. Kwa sababu yeye ni kiongozi shupavu, ajaribu kurudisha haki za binadamu. Kama kuna watu walishikwa kwa sababu ya siasa, waachiliwe. Katika Hotuba yake, nilisoma kuwa anaheshimu Bunge la Kenya na Kenya kwa ujumla, kwa sababu ya upana wa demokrasia yetu. Tunataka pia kuona upana wa demokrasia ya Tanzania. Tunawatakia kila la heri. Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Ninafikiri kuwa kuna wale ambao hawakuwa wanatarajia kuwa ninaweza kuongea Kiswahili sanifu. Ningependa kuwahakikishia kwamba Kiswahili ambacho nimeongea hapa ni cha hali ya juu. Ninatarajia kuwa katika siku za usoni tutakuwa tunafanya mijadala ya Bunge, Miswada na mambo ya sheria kwa Kiswahili. Wakenya waelewe Kiswahili kwa sababu kinafaa kutukuzwa. Tulifunzwa kuanzia shule za msingi, shule ya upili na vyuo vikuu. Nafikiri kuwa lugha ya Kiswahili inaweza kueleweka kwa Wakenya wote, haswa kwenye vitongoji na ofisi kubwa. Ningependa kuwarai Maseneta wajaribu kuongea Kiswahili. Nitabaki hapa nimsikize Mwenyeketi wa Kamati ya Sheria, Ulinzi, na Haki za Binadamu, ambaye nilikuwa mtangulizi wake, aongee Kiwahili sanifu ili tupate fursa ya kunufaika. Kufikia hapo, ninakushukuru. Ninaunga mkono na kumtakia Rais wa sita wa nchi ya Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kila la heri. Pia ninaomba kuona Tanzania inaendelea kidemokrasia na katika maswala ya haki za kibinadamu na undugu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki."
}