GET /api/v0.1/hansard/entries/1073075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1073075,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073075/?format=api",
"text_counter": 249,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omogeni",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13219,
"legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
"slug": "erick-okongo-mogeni"
},
"content": "Ninaungana na Maseneta waliyozungumza mbeleni kumpongeza Rais Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pili, ninampongeza kwa kuanzisha urafiki na ujirani mwema na Taifa la Kenya kwa kututembelea. Waswahili husema: “Fimbo ya mbali haiui nyoka”. Hivyo basi, tukiwa na jirani ambaye ni Tanzania na tunahusiana vizuri, ni wazi kwamba tunaweza kumtegemea. Uhusiano wa hizi nchi mbili unaweza kuleta manufaa sana."
}