GET /api/v0.1/hansard/entries/1073079/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1073079,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073079/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omogeni",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13219,
"legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
"slug": "erick-okongo-mogeni"
},
"content": "Isitoshe, ninamshukuru Rais Mhe. Suluhu Hassan kwa mambo aliyozungumzia katika Hotuba yake. Ninampongeza kwa kuwa mstari wa mbele kutambua kwamba janga la COVID-19 limeleta madhara makubwa kwa watu wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Alizidi kusema tuungane sote kama Jumuiya, ili kuhakikisha tunapigana na janga hili lililosababisha matatizo mengi. Alihimiza haya mataifa mawili yapime wananchi wanaovuka mpaka wa Kenya na Tanzania ili kuhakikisha hakuna kusambaza hivi virusi. Rais Suluhu alitambua kwamba tusipoweka jitihada za kupambana na hili janga la COVID-19, huenda litatusababishia madhara makubwa sana. Tunapoangalia Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni vizuri pia tuangalie jinsi jumuiya zingine zimefaidika kwa kuwa na uhusiano wa karibu wa kiuchumi. Jumuiya ya Mataifa ya Ulaya imeweka mikakati ya biashara miongoni mwao. Watu wanaoishi katika hiyo Jumuiya, wanafanya biashara kana kwamba ni watu wa nchi moja. Watu wanatoka taifa moja hadi jingine kana kwamba wako katika taifa moja. Ninamshukuru Rais Suluhu kwa kutukumbusha kwamba sisi ni mandugu. Nilipokuwa katika shule ya upili, nilifundishwa Kiswahili na mwalimu kwa jina Bw. Peter Joseph, ambaye alikuwa Mtanzania. Alikuwa amebobea katika lugha ya Kiswahili. Wakati huo, Kenya haikuwa na walimu wa kutosha na ndio tukachukua walimu kutoka Taifa jirani la Tanzania. Ninakumbuka pia katika somo la Kiingereza, tulikuwa na mwalimu kutoka taifa jirani la Uganda. Kwa hivyo, sisi kama mandugu, tunahitaji kushirikiana na kufanya kazi pamoja. Tunapaswa kutambua kwamba mipaka ililyowekwa na Wakoloni haitakiwi kututengenisha. Zipo faida nyingi ambazo tutapata, ikiwa tutazidi kukuza uhusiano ambao tumekuwa nao kwa miaka mingi. Rais Suluhu alikuja tu kutukumbusha kwamba ni vizuri tuongeze jitihada kuhakikisha tunaboresha uhusiano uliopo baina ya mataifa yetu. Sisi na Tanzania tunafanya biashara. Magari mengi kutoka Kenya husafirisha bidhaa hadi Tanzania. Kwa hivyo, tukiwa na uhusiano mwema, wafanyibiashara watakuwa na nafasi nzuri sana na kuendeleza biashara zao. Rais Suluhu pia aligusia maswala ya utalii. Alieleza jinsi wanyama pori hutembea kati ya hizi nchi mbili. Mara wanatoka Tanzania na kuingia Pori la Maasai Mara huku Kenya, halafu wanarudi Tanzania. Tukitunza haya mataifa yetu, tutaendelea kudumisha uchumi wetu wa kiutalii. Tunaweza hata kujenga reli kutoka Mombasa kuja hapa Nairobi, ielekee Malaba, Uganda na hatimaye Tanzania. Hivyo ndivyo usafiri ulivyo katika Jumuiya ya Ulaya. Wakati mmoja nilikuwa Ulaya na nikapanda gari la moshi kutoka Ufaransa, nikapita Ubelgiji na hatimaye Uholanzi. Ningependa Jumuiya ya Afrika Mashariki tujitahidi sana na hii reli yetu itoke Mombasa kuja hapa Nairobi, iende Nakuru na hata ipite Malaba na kupenyeza mataifa yote ya Afrika Mashariki. Ninawapongeza Marais, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Suluhu Hassan wa Tanzania. Ninawaomba marais wa mataifa mengine waige mfano mwema uliowekwa na"
}