GET /api/v0.1/hansard/entries/1073081/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1073081,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073081/?format=api",
"text_counter": 255,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omogeni",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13219,
"legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
"slug": "erick-okongo-mogeni"
},
"content": "hawa marais wawili. Wamejiweka mstari wa mbele kustawisha uhusiano wa karibu na kuboresha biashara na uchumi baina ya mataifa yetu mawili. Nikimalizia, ikiwa hizi nchi zetu zitakuja pamoja, hata kupigana na ufisadi itakuwa rahisi. Tukiwa na uhusiano mzuri, itawezekana kubadilisha habari za ujasusi kati ya mataifa yetu na haswa Jumuiya nzima ya Afrika Mashariki. Bi Spika wa Muda ninakupongeza wewe pia kwa sababu umeangazia sana faida tunazoweza kupata tukiwa na uhusiano mwema na Tanzania. Ninakumbuka nilipokuwa Mwenyekiti wa Shirika la Wanasheria nchini Kenya, tulisafiri hadi Uganda kukutana na Rais wa Uganda, Kaguta Yoweri Museveni na tukakubaliana kwamba mawakili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wawe na uhuru wa kufanya biashara yao katika mataifa yao. Sisi tuliporudi nyumbani tulienda tukachapisha nakala maalum katika ile Kenya"
}