GET /api/v0.1/hansard/entries/1074333/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1074333,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1074333/?format=api",
"text_counter": 294,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Poghisio",
"speaker_title": "The Senate Majority Leader",
"speaker": {
"id": 202,
"legal_name": "Samuel Losuron Poghisio",
"slug": "samuel-poghisio"
},
"content": "Rais wetu, Rais Uhuru Kenyatta, kwa kumualika na kupatia fursa na ruhusa ya kupata kiongozi mgeni kuja kuhutubia. Kikao cha pamoja ambacho alihutubia katika Bunge kilifana sana. Ningependa kuwashukuru Wabunge wenzangu, Maseneta, ambao wamejaribu kujadili kwa Kiswahili. Wengi hawajafanya hivyo lakini naomba kwamba tukipata nafasi ama fursa nyingine, tungehimiza kwamba Maseneta wote wachangie kwa lugha ya Kiswahili. Bi. Naibu Spika pia ningeomba kwamba ile harakati yetu ya kutafsiri Kanuni zetu za Bunge katika lugha ya Kiswahili imalizwe kwa haraka, ili pia tuchukue siku moja katika wiki kujadili kwa lugha ya Kiswahili. Bi. Naibu Spika, kwa hayo machache, nawashukuru Maseneta wote na kuomba kujibu."
}