GET /api/v0.1/hansard/entries/1074375/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1074375,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1074375/?format=api",
    "text_counter": 36,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika kwa kunipa hii nafasi ili kupitisha salamu za faraja kwa familia na wana Nairobi kwa ujumla, kwa kumpoteza mchezaji mashuhuri wa raga, Bw. Benjamin Ayimba. Yeye alifanya bidii akiwa mwanamchezo mashuhuri wa raga na alichangia pakubwa kuweka jina la Kenya katika ramani ya dunia. Bw. Ayimba alikuwa ni mkufunzi mzuri ambaye alikuwa na nidhamu na nguvu kama mchezaji, ambaye nguvu zake ni za kuigwa. Nikiwa mimi ni mkufunzi wa mchezo wa kandanda na kama wakufunzi wa michezo mbalimbali, tunafanya kazi kubwa sana kuhakikisha kwamba wanamchezo wanapata ujuzi wa kucheza lakini kando na ujuzi peke yake, kuna yale mengine yanayo funzwa pale uwanjani. Kwa mfano, nidhamu ya hali ya juu. Bw. Ayimba alikuwa na nidhamu ya hali ya juu na aliweza kupitisha hio nidhamu kwa wachezaji wengine. Wakati alifanya bidii kuinua wengine katika kiwango kile chake na wale wachezaji walipata kipato kizuri kupitia kwa huu mchezo wa raga. Kwa hivyo, napenda kuungana na Wakenya na wanamchezo wengine nikiwa kama Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Michezo na Leba, niseme kwamba tusaidiane na tushikane mikono na familia ya Benjamin Ayimba ili kuhakikisha kwamba huu mchezo wa raga umefika kiwango kingine. Bw. Spika, sio mchezo wa raga peke yake lakini michezo mingine. Kenya inapata kipato cha juu kupitia kwa michezo kama raga na mbio ambazo tunaangalia wenzetu wanaotoka Bonde la Ufa. Wameleta kipato cha hali ya juu sana. Nashukuru pia wale viongozi ambao tumesikia kwa Mwenyekiti wa Kamati la Michezo na Leba kwamba walichangia pakubwa kulipia malipo ya hospitali ya Bw. Ayimba alipokuwa hospitalini. Kwa hivyo, sisi wengine sote tushikane mikono ili tusaidie familia na kuhakikisha ya kwamba Benjamin Ayimba tumempa buriani ya heshima na tunaomba Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi."
}