GET /api/v0.1/hansard/entries/1074798/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1074798,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1074798/?format=api",
    "text_counter": 253,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kuanzia mwanzo, nataka kusema ya kwamba naunga mkono mji wa Nakuru ufanywe jiji kwa sababu mimi nilikua mwenyekiti wa Standing Committee on Devolution and Intergovernmental Relations,Kamati ambayo tulishughulikia maswala haya kwa mapana na marefu. Ukweli usemwe; nataka kumshukuru Sen. Kihika kwa sababu alijifunga kibwebwe na akasema ni mpaka tuangalie haya maswala kwa kindani kulingana na sheria iliyo katika Katiba yetu. Katiba ya Kenya inasema kwamba kulingana na mambo ambayo yanapaswa kufuatiliwa, Nakuru imeweza kujikimu kikatiba na kwa hivyo hatuna lolote ila kuifanya iwe Jiji. Bw. Spika, ukizingatia idadi ya watu, jiji inapaswa kuwa na idadi ya watu wanaozaidi laki mbili na nusu na Nakuru ina zaidi ya watu laki tatu."
}