GET /api/v0.1/hansard/entries/1074799/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1074799,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1074799/?format=api",
"text_counter": 254,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Ukiangalia mambo ya usafi wa mazingira, nilipigwa na butwaa kuliposemwa kwamba Nakuru hawajazingatia hayo. Niliopotemebea kule, niliona kwamba kiyesi chochote kinachopelekwa upande wa chini kinatumika kutengeneza makaa. Tulitembea huko na Sen. Nyamunga na marehemu Sen. (Dr.) Kabaka, Mungu amlaze pahali pema peponi. Tulinunua makaa hiyo na kujionea kuwa inafanya kazi safi kabisa. Serikali ya Kaunti ya Nakuru inafanya kazi nzuri katika kuhifadhi mazingira. Tulitembea mahali panaitwa Gioto kule Kiamburu kunakokusanywa takataka, Tuliona kwamba wanafanya tulivyowashauri katika kumudu takataka zao. Takataka zilikuwa zimekusanywa vizuri na tayari walikua wanatumia ile ardhi kupanda miti. Bw. Spika, kwa upande wa afya, tulitembelea hospitali moja ambayo imetenga sehemu ya ujenzi wa wadi za kina mama na wengine kulazwa. Mradi huo utawagharimu zaidi ya milioni mia sita. Kwa hivyo, ninaunga hoja hii mkono. Upande wa barabara, walituonyesha yale mambo wanapanga kufanya. Walikua wameshaa pitisha mipango za ujenzi katika bunge lao la kaunti na walikubaliana katika mikakati ya kutimiza mipango hiyo. Tulitembelea kituo cha zima moto na walituonyesha jinsi vituo hivyo vitakua vikifanya kazi. Walikua wamesha jitayarisha kwa mambo yale. Bw. Spika, jambo ambalo lilikua kizingumkuti ni ile ya watoto wa mitaani waliondelewa na kaunti ya Nakuru. Hilo ndilo jambo nitakashifu kwa sababu---"
}