GET /api/v0.1/hansard/entries/1074823/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1074823,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1074823/?format=api",
"text_counter": 278,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "La haula ni vizuri niseme kwamba tungependa huu mji uwe mji mkuu lakini usifanywe kuwa mji mkuu sasa hivi. Kwa sababu ninapo ongea huku, kuna ripoti ya Kamati ya Kazi na Ustawii wa Jamii ambayo ni kamati ya Nyumba hii. Nikiwa ni naibu wa mwenyekii wa hiyo kamati, tuko na pendekezo la kusema kwamba hatungependelea kwa sasa ule mji wa Nakuru kuwa mji mkuu kwa sababu ya matukio yaliyotokea kule Nakuru ya kutoa watoto wadogo na zile familia za mijini na kuwatupa katika misitu. Bw. Spika, kwa hivyo wakati mara kwa mara tunapokuwa na Maombi ama petitions za wananchi wetu, wakati tumeandika ripoti ya kamati, Clerk wa Seneti huwa anaandika barua na kupeana ile ripoti kwa taasisi ili yale mapendekezo yatimizwe. Hapo sasa ndio nina shida. Wale watu wa Nakuru walioandika Petition kwa hii Nyumba wako na mapendekezo ambayo mengine yanatakikana kutimizwa na Nyumba hii ya Seneti. Pendekezo moja ni kwamba tusipeane ule mji wa Nakuru hali ya mji kuu kwa sasa mpaka watuhakikishie kwamba kuna miundo msingi ama miundo mbinu ya kuhakikisha kwamba wale wananchi wote wanaoishi mji wa Nakuru ikiwa ni walala hoi ama walala hai, masikini ama tajiri, watapatiwa nafasi yao ya kuishi mji wa Nakuru bila kutatizwa na mtu. Bw. Spika, tuliuliza kama Kamati ya Kazi na Ustawi wa Jamii kama serikali ya Nakuru inaweza kutoa na kutupa wananchi wao wenyewe kule msituni na haijakuwa mji bado na hawajaunda miundo mbinu ya kuhakikisha kwamba hawa watoto wanaishi kwa mazingira yanayofaa; je tukiwapatia hali ya mji, si ndio watawatupilia mbali zaidi? Kwa hivyo naomba wenzangu wanikubalie kwamba kwa sasa hivi tuangushe huu Mswada alafu tupeane serikali ya Nakuru muda kidogo ili wajifahamu na wajielewe; waunde miundo mbinu ya kutosha ya kuhakikisha kwamba mwananchi yeyote anayeishi Nakuru ako na haki sawa na yule mwingine awe masikini ama tajiri. Kwa sababu vile Sen. Mutula Kilonzo Jnr. amesema, wale wananchi waliotupwa porini na wengine wakaliwa na wanyama, wako na haki kama sisi wengine. Tukitoa damu yao na yetu yote ni nyekundu. Bw. Spika, kwa hivyo ningependa kusihi wenzangu kwa sababu tuko na ripoti tayari. Sen. Sakaja amejaribu kuingia kupitia mtandaoni lakini hajafaulu. Kwa niaba ya kamati yangu, naomba kwamba tuangushe huu Mswada kwa leo, tuipatie serikali ya Nakuru nafasi wajielewe na wapate ufahamu wa kulea watu wao vizuri alafu kwa muda mwingine ujao wa usoni tupitishe huu Mswada wa kuwa na hali ya mji. Hakuna mtu ambaye hataku kuwa na mji. Zamani kwetu tukitoka kule Taita---"
}