GET /api/v0.1/hansard/entries/1075450/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1075450,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1075450/?format=api",
"text_counter": 46,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia ardhilhali ya Bw. Mageuzi. Kusema kweli, ufisadi umekithiri katika serikali za ugatuzi. Ninakubaliana na Sen. Wambua aliposema kwamba tuligatua ufisadi; kwamba kati ya yale mambo ambayo tuligatua, kubwa zaidi ilikuwa ufisadi. Ufisadi umekithiri katika serikali za ugatuzi, na ninashukuru kwa sababu wananchi wameanza kuona kuwa sio lazima uangalizi ufanywe na mabunge za kaunti. Wananchi wenyewe wanaweza kuchukua hatua kuhakikisha kwamba uangalizi umefanywa vizuri. Kusema kweli, katika serikali za ugatuzi, ufisadi umepewa kipaumbele. Fedha zinazoenda kusaidia wananchi haziwafikii na kutumiwa kwa lengo lililokusudiwa. Nakubaliana na wenzangu waliosema kwamba kuna miradi mingi ambayo imeanza katika ugatuzi na haijakamilika kwa sababu ya ufisadi. Katika Kaunti ya Taita Taveta, kuna miradi mingi ilyoanzishwa. Kwa mfano, wakati wa mambo ya COVID-19, kuna"
}