GET /api/v0.1/hansard/entries/1075452/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1075452,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1075452/?format=api",
"text_counter": 48,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "ambazo zilikuwa zinajengwa. Baada ya kupata Ksh153 milioni zikiwa pesa za COVID-19, bado hiyo hospitali haijakamilishwa mpaka leo. Laini ya kwanza ya uangalizi ni ya wajumbe wa kaunti kwa sababu mara kwa mara kunapotokea ufisadi, wananchi wanaangalia Seneti sana. Ninashukuru kwa hiyo imani wananchi walio nayo kwa Seneti kufanya uangalizi. Lakini uangalizi wa kwanza unatakikana kufanywa na mabunge ya kaunti . Bi. Naibu Spika, la kusikitisha ni kwamba wajumbe wa serikali za kaunti wamenunuliwa na kuwekwa kwa mfuko na magavana. Sasa hakuna uangalizi wa kutosha unaofanyika katika serikali za ugatuzi. Kwa hivyo, ninawaomba wananchi ambao wako kule mashinani wachukue hatua mikononi mwao, kama hawajaridhika na uangalizi unaoendelea katika mabunge ya kaunti. Inafaa wawasilishe ardhilhali zao kwenye Seneti, na sisi tutaangalia jinsi tutakavyoendelea. Tutafuatilia kuona vile hii petition itakavyoenda ili ya Bw. Mageuzi apate majibu yake ndani ya siku 60 kwa hiyo ardhilhali na watu wa Kisii wapate afueni kwa hayo maswala yaliyoibuka na Bw. Mageuzi. Asante, Bi. Naibu Spika, kwa hii nafasi."
}