GET /api/v0.1/hansard/entries/1075904/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1075904,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1075904/?format=api",
    "text_counter": 38,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Yes, Sir. Mhe. Spika, ningeomba nikariri kilio hiki kwa Kiswahili ili tuweze kufahamikiana. Niko na Ardhilhali ya umma, ambayo kwa lugha maarufu ni Public Petition, Nambari 22 ya 2021. Tukitukuze Kiswahili kiongozi wangu ili tufahamikiane hapa na nje ya Bunge pia. Ardhilhali Nambari 22 ya mwaka 2021 inayohusu pingamizi za biashara mjini Mombasa. Mhe. Spika, mimi, Mhe. Abdullswamad Nassir, Mbunge wa eneo la Mvita, kwa niaba ya wafanyibiashara katika Kaunti ya Mombasa na hususan wafanyibiashara wadogo katika Mama Ngina Water Front, kwa jina jingine Light House, na Jomo Kenyatta Public Beach ama kama inavyojulikana Bamburi Beach, nataka kufahamisha Jumba hili mambo yafuatayo: Kwanza, Wizara ya Utalii, kwa madai inayosemekana ni ilani kutoka kwa Wizara ya Afya, waliamrisha kufungwa kwa Mama Ngina Water Front na Jomo Kenyatta Public Beach kwa madai ya maradhi ya coronavirus . Mamia ya wafanyibiashara wa maeneo ya Mama Ngina Water Front na Jomo Kenyatta Public Beach kwa sasa wanapoteza mapato yao na familia zao baada ya kuzuiwa kuingia na kufanya biashara katika sehemu hizo. Wafanyibiashara hao wameteseka mno. Biashara zao ni vitu, kwa wale wenye kufahamu, kama kachiri, madafu, mihogo, kutembeza watu katika sehemu hizi za utalii kwa maboti, wauzaji ushanga na mavazi ya bahari. Wafanyibiashara hawa wamekuwa katika sehemu hizi zaidi ya miaka arobaini na hawana pengine pa kwenda. Hii inasababisha ufukara, kukosa kutazama familia zao, kusomesha watoto wao na, mwishowe, uhalifu utazidi. Mhe. Spika, tunafurahi na kukubali ya kuwa baadhi ya sehemu nyingine ya biashara Kubwa kubwa kuweza kufunguliwa, lakini tusiwe ni wenye kusahau ya kuwa tunafungua zile kubwa ilhali wale ambao ni wenye biashara ndogo ndogo wanaumia. Wafanyibiashara hawa wamejaribu kila njia kuzungumza na wenye kusimamia maeneo haya na kilio chao kimeenda pahali ambapo hawajaweza kuridhika. Nataka kukariri vilevile ya kuwa haya maswala ambayo nimeweza kuyaleta katika bunge hili hayapo mbele ya korti yoyote ya sheria hii Kenya."
}