GET /api/v0.1/hansard/entries/1076110/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1076110,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1076110/?format=api",
    "text_counter": 244,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": "Hili si jambo la kwanza kuwahi kutajwa katika Bunge hili. Utakumbuka, Mhe, Spika, nikikurudisha nyuma, wakati ambapo kulikuwa na masuala ya sukari. Baadhi ya Wabunge walisema kwamba wapo wenzao waliopokea baina ya Kshs10,000 na Kshs30,000 ndani ya choo ili wapitishe masuala fulani katika Bunge hili. Kwa hivyo, kwa Mbunge mwenzangu kusimama na kunitaja mimi Mohamed Ali bila ushahidi tosha, inaonekana kwamba ni kupelekwa katika... Kwanza, sijui ni nani alisema mimi, Mohamed Ali, nilizungumza katika hili Bunge na kusema mambo hayo. Ningependa kujua. Ndiyo maana nilipokuandikia barua nilitoa ombi la kusema itakuwa vyema nikijua ni nani ili niweze kujibu kulingana na masuala aliyouliza. Ingawa hivyo, muda umeyoyoma. Ni wakati muhimu kusonga mbele. Tugange yajayo ili tuendeleze nchi hii. Tuwasaidie wananchi kwa kutunga sheria."
}