GET /api/v0.1/hansard/entries/1076783/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1076783,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1076783/?format=api",
    "text_counter": 528,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Katika hiki kitengo cha kwanza cha Executive Office of the President, wanafaa kupewa pesa zaidi na hata hicho kipeo chao kinafaa kuongezwa juu zaidi kwa sababu kinafanya kazi nyingi nzuri. Katika State Department of Interior and Citizen Services, kipeo chao kikipelekwa juu zaidi itakuwa vizuri kwa sababu bado tunatarajia kazi iwe nzuri zaidi. Hii ni kwa sababu kuna sehemu zingine kama kule kwetu, Kaunti ya Lamu, bado kuna watu hawajapata vitambulisho kwa miaka mitatu sasa. Wanazo stakabadhi zile za kungojea vitambulisho. Kama hiyo pesa ni kidogo, kazi haifanyiki vizuri. Kwa hivyo, hata wakiongezewa siyo vibaya. Bora kazi ifanyike. Sisi watu wa Lamu pia ni Wakenya kama Wakenya wengine. Kwa hivyo, ule muda ambao unamchukua mtu wa Nairobi kupata kitambulisho ndio unafaa achukuwe mtu wa Lamu kupata kitambulisho. Ningependa pia kuzungumzia Wizara ya Ulinzi. Kusema kweli, sisi kule Lamu ndio tunaona kazi yao kwa vile tuko katika mpaka. Wanafanya kazi nzuri na huwa tunawatarajia kutupitisha katika sehemu zingine ambazo hatuwezi pita pekee yetu. Kwa hivyo, kama kuna pesa zinatakikana, wapewe hata zaidi. Kazi yao ni nzuri na tunawapongeza sana. Ningependa kuzungumzia kuhusu maji. Maji ni uhai. Hii Wizara ya Maji, Usafi na Umwagiliaji hata wakiomba pesa nyingi wanafaa wapewe. Kipeo chao kinafaa kuenda juu ili wapate kuomba hata nyingi zaidi kwa sababu bado kuna sehemu zingine hapa Kenya ambazo watu bado wako na matatizo ya maji. Tunajua maji ni muhimu kwa binadamu. Huko Lamu kuna mipango ambayo imekua kwenye vitabu zaidi ya miaka kumi ya kuvuta maji kutoka Mto Tana mpaka Lamu. Kwa hivyo, wanatarajia kuwa katika mipango hiyo. Hizi pesa wameomba zitashughulikia maslahi ya Lamu kwa sababu ilikuwa katika mipango. Wakiweza kuleta maji Lamu basi tutakuwa tumetatua matatizo ambayo tuko nayo huko. Tatizo letu kubwa zaidi hivi sasa ni ukosefu wa maji. Bandari iko na wageni watakuja wengi lakini tuko na shida ya maji. Wageni wakija wengi zaidi, hatutakuwa na maji. Hata hivyo, naona Rais alizungumzia jambo hilo alipokuwa Lamu. Waziri pia alizungumza na tumeona katika magazeti. Rais alituambia kwamba wataangalia vile watasaidia upande wa maji ili tuweze kijipanga na ile Bandari ya Lamu. Nataka kuzungumza kuhusu afya. Hizi pesa zilizopangwa kwa afya, wenzangu watakubaliana nami kuwa zinafaa kupangwa zaidi kwa sababu afya ndiyo kila kitu. Tukizingatia afya hapa Kenya, basi tutakuwa tumebadilisha maisha ya binadamu kwa sababu afya inaingilia pande nyingi. Sikuwa naelewa ni vipi Wizara ya Afya na Wizara ya Uchukuzi, Miundombinu, Makazi, Maendeleo ya Mijini na Ujenzi wa Miradi ya Umma zinaweza kuingiliana lakini baada ya kupelekwa kusoma, tumeona afya iko kila upande. Hata Bungeni afya iko. Ukienda kwa usafirishaji, afya iko. Afya iko kila mahali! Kwa hivyo tukizingatia afya, tutakuwa tumetatua shida za Wakenya. Kwa hiyo, sekta ya afya inafaa iangaliwe vizuri na ipewe pesa nzuri lakini pia wale ambao wanashika hizo pesa wanafaa kuzitumia inavyotakikana ili tusije tukaharibiana majina. Naibu Spika wa Muda, ninasikitishwa kidogo pia na Wizara ya Kilimo upande wa blue"
}