GET /api/v0.1/hansard/entries/1076944/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1076944,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1076944/?format=api",
"text_counter": 150,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Asante sana Mhe. Spika. Kupitia Kanuni za Kudumu 44(2)(c), naomba kupata jawabu kutoka kwa kamati husika ya Elimu kuhusu mambo ya Serikali kulipia wanafunzi wa shule za upili karo. Serikali iliweka mikakati kulipia wanafunzi wa shule za upili mwaka wa 2008 ili kuhakikisha kila mtoto anaweza kupata elimu licha ya kipato cha jamii yake. Hali hii ilisababisha wanafunzi kuwa wengi na kuongezeka katika shule zetu. La kusikitisha, Waziri wa Elimu, juzi ametoa amri kwa walimu wakuu wa shule hizi kufukuza wanafunzi ambao wana deni la karo. Hakuachia hapo. Alidai kuwa wazazi hawalipi karo kusudi licha ya kuwa wana uwezo. Matamshi haya ambayo ni ya kusikitisha, ya kushangaza na ya kukemewa yamezua utata kuhusu mpangilio wa kuhakikisha asilimia 100 ya wanafunzi wanaweza kuingia shule za upili. Wazazi wana shida haswa sasa ambapo uchumi umezoroteshwa na mambo ya Corona. Pesa za NG-CDF ambazo zafaa kusaidia kulipa karo hazijatoka ipasavyo. Wazazi na wanafunzi hawa watasaidika vipi? Kwa haya, twahitaji jawabu au majawabu kwa masuali yafuatayo: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}