GET /api/v0.1/hansard/entries/1076949/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1076949,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1076949/?format=api",
"text_counter": 155,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Tatizo si wiki mbili. Tatizo ni ombi letu. Nina imani kuwa wale wenye kufikisha habari hizi kwa Serikali wanajua kwamba watoto wetu kila wakikaa nje ya shule inawawia rahisi kuingia katika uhalifu. Watoto hawa hawa ndio wataingia katika mambo yasiyofaa kijamii. Kwa hivyo, tukumbuke kuwa wiki mbili hizi ni mamilioni ya watoto ambao watapoteza maisha yao na ni lazima mtu aweze kuchukua jukumu. Kwa hivyo itakuwa ni bora apunguze ili tujue msimamo ni wa Serikali au mtu binafsi."
}