GET /api/v0.1/hansard/entries/1077399/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1077399,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1077399/?format=api",
"text_counter": 111,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi na mimi nichangie. Naunga mkono kaunti zipate pesa. Lakini kaunti zikipata pesa hizo, zilipe madeni yao kwanza. Kama wenzangu walivyotangulia kuzungumza, wanakandarasi wengi wanapata shida. Wengine walichukua mikopo na wengine pia wana familia. Kwa hivyo, ni muhimu mwanzo wawalipe kisha waendelee na mengine. Pia, nizungumze kuhusu pesa zinazostahili kupelekwa kwa pensheni. Kaunti zinafaa zipeleke pesa hizo mwanzo. Ni kwa sababu wao wanakata kwa wafanyakazi kisha hawazipeleki kule. Hiyo ni kama kombora ambalo linangojea kupasuka. Itafika wakati wale wafanyakazi wa kaunti hawatalipwa pensheni yao. Hiyo itakuwa ni vibaya sana kwa sababu mtu amefanya kazi akitoa jasho lake na kujua amejipanga akienda uzeeni. Kisha, aende akose pesa hizo. Imekuwa shida kwa haya mashirika ya pensheni kwa sababu wanaomba kaunti wawalipe, hawalipi. Na si kaunti zote. Kuna kaunti zinalipa vizuri lakini kuna kaunti hazilipi. Labda hapa itatubidi tutunge sheria ili zile kaunti hazilipi basi wafanyakazi wao wasilipwe. Ni kwa sababu kuna kaunti zingine zinachukua na kukimbia kulipa na wanaona wafanyakazi wao wanalipwa. Labda tutunge sheria ili pesa za pensheni zikatwe kabla hazijafika kwa kaunti au wafanyikazi ambao kaunti zao hazilipi wasilipwe. Maanake hii ni shida kubwa na italeta shida kwa wafanyakazi wa kaunti. Nikizungumzia upande wa ile formula inatumika hapa, mwanzo ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu na nimshukuru Rais wetu Uhuru Kenyatta kwa sababu ya kujenga bandari ya Lamu. Sisi hapa kilio changu kimesikika. Siku zote nikiwa hapa nang’ang’ania na nasikia uchungu watu wakisema kwamba wako wengi na sisi tuko wachache. Nikiona uchungu tukiambiwa tuko wachache. Nashukuru kwa hii Poti ya Lamu kujengwa. Hili la kusema tuko wachache litaenda kwenye kaburi la sahau. Sasa wengine watalia wao kwa sababu mtakuja kule Poti ya Lamu na tutakuwa na watu wengi na hesabu ni yetu. Inshallah, mgao huu utaweza kuja kwa formula hii. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}