GET /api/v0.1/hansard/entries/1077400/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1077400,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1077400/?format=api",
"text_counter": 112,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Itatusaidia sisi muliokuwa mkituona wachache. Saa hii inshallah, tutakuwa wengi Mungu akipenda. Kaunti wakipata pesa hizi wahakikishe wamezitumia vizuri kwa afya, kwa sababu afya ni kwa kila kitu. Pia, watumie nafasi hiyo kwenda kuhamasisha na kuwaeleza wananchi, haswa akina mama, mambo ya afya. Afya sio kujenga hospitali tu bali pia kujua huduma zinazopeanwa. Kuna changamoto sehemu za kwetu. Kuna watu hawafikii zile hospitali. Hospitali kama ya King Fahd iliyoko pale, kutoka Kiunga mpaka kule ni Kshs2000. Sasa tunawaomba hawa Magavana wahakikishe kila wodi imefikiwa. Kwetu haiendi hata kwa wodi. Kama wodi ya Kiunga, Ndau na Kiwayu iko kwa wodi moja na ni Kiunga. Hospitali kubwa ikiwa Kiunga haimsaidii mtu wa Ndau. Itabidi yule mtu wa Ndau afadhali aende Lamu kuliko kurudi Kiunga. Kwa hivyo, sehemu zetu zina changamoto za usafiri. Hawa magavana wamepewa hii nafasi maanake kila ukitaka kuzungumzia afya wanakuambia hii si kazi yako. Lakini, ni kazi yao. Basi wafanye ile inayostahili kufanyika angalau hivi visiwa vipate huduma nzuri ya afya. Maanake ikiwa kama kwenye kisiwa hakuna daktari, huwa ni shida sana. Inabidi watu wasafiri wakizidiwa na magonjwa usiku au bahari ni chafu. Hivyo si sawa. Kila mtu anafaa ajihisi ni Mkenya na zile huduma zimfikie alipo. Upande wa maji, maji ni uhai na tunasema siku zote. Magavana wamepewa nafasi. Twajua pia sisi wa Serikali Kuu tuna nafasi na majukumu yetu. Tunang’ang’ana kwa upande wetu, lakini kaunti wao wamepewa hii nafasi. Sisi hata tuking’ang’ana kwa Serikali Kuu, kisha hupewa wao kufanya. Kwa hivyo, tunawaomba magavana, wakipewa pesa hizi, wazitumie vizuri na maji yawafikie watu. Wanaopata shida zaidi ni akina mama na watoto. Ikiwa mwanamke ataulizwa, badala ya kujenga ataenda kwenye maji na afya. Lakini wengi wa magavana ni wanaume ndio maana tunataka tubadilishe hawa magavana wengi wawe wanawake maanake wanawake ndio wanafikiria sana hizi huduma kuliko wanaume. Wanaume wanataka kujenga, kujenga, kujenga. Asante Bi. Spika. Kuna mengi ya kuzungumza lakini wacha niwapatie wenzangu nafasi wazungumze."
}