GET /api/v0.1/hansard/entries/1077980/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1077980,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1077980/?format=api",
"text_counter": 104,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Maridhiano yalikuwa yawe tangu Novemba 2019 lakini maridhiano hayo yakakubalika hadi Januari 2020. Yatia wasiwasi ya kuwa tangu Januari 2020 mpaka leo mishahara hiyo ambayo iliweza kukubaliana na kuridhiana pamoja haijalipwa. Kuna haja ya kuanza mazungumzo ya maridhiano ya 2022/2023 ambayo, kisheria, yanafaa kuanza Oktoba 2021 pamoja na kurejeshwa kazini kwa wale wafanyikazi 247. Kutokana na hayo, natafuta suluhisho kupitia kwa Mwenyekiti husika. Kwanza, atueleze ni mitihani gani ambayo inasababisha kutotekelezwa kwa hii CBA hadi leo. Pili, ni mikakati gani Wizara imeweka kuhusu hii CBA ama maridhiano ya 2022/2023 yanayofaa kuanza mwaka huu na hadi leo, yale ya mwaka 2019/2020 hayajatekelezwa. Tunaomba Mwenyekiti atoe hakikisho kuwa wizara husika itahakikisha mishahara ya hawa wafanyikazi ambao ni wana Mombasa na Wakenya, kwa jumla zaidi ya 5,000, yaanze Januari 2020 kama vile ilivyo. Ni haki yao kulipwa mishahara hiyo tangu Januari 2020 na wahakikishe ya kuwa wafanyikazi 247 waliofutwa mwaka 2011 warejeshwe."
}