GET /api/v0.1/hansard/entries/1078013/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1078013,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1078013/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mwatate, ODM",
"speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Kwa kweli, hili tatizo limeenea pembe zote za Taita Taveta. Kule sehemu za Mwatate katikati ya Kaunti ya Taita Taveta, sehemu za kigombo mahali kunaitwa Mwanda na Kituma, mamia ya ndovu walikuwa huko leo asubuhi. Hata ilikuwa ni vigumu kwa watoto kuelekea shuleni asubuhi. Tumezungumza kuhusu hili tatizo kwa muda. Sijui tutafanya aje mpaka hili tatizo litatuliwe, kwa sababu Jimbo la Taita Taveta limezingirwa na mbuga za Wanyama za Tsavo West na Tsavo East. Matatizo yamekuwa mengi sana."
}