GET /api/v0.1/hansard/entries/1078374/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1078374,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1078374/?format=api",
"text_counter": 498,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Vile vile, ni jambo muhimu sana na ni jambo linalohitaji kuzingatiwa, kwamba, zile fedha ambazo zinaenda katika serikali gatuzi, ni fedha ambazo zinahitaji kuwahudumia wananchi. Lakini kwa masikitiko makubwa, tumeweza kushuhudia kwa takriban hivi sasa awamu ya pili kuanzia serikali hizi zianze shughuli zake, kwamba kumekuwa na matatizo mengi sana, husasan katika zile hali za uongozi ambao unapatikana katika sehemu hizo. Mbali na maadhimiyo ya Wakenya kutaka serikali za kaunti ziwe zinafanya kazi katika sehemu 47 zilizopo, yale yanayoshuhudiwa hivi sasa yamekuwa ni matatizo mengi sana. Ukweli ni kwamba Wakenya wanahitaji huduma lakini zile shida na mateso yanayoonekana hivi sasa yanasikitisha sana. Mfano, utapata kwamba wakati mwingine inafika hadi miezi mitatu au minne wafanyikazi wa kaunti hawajalipwa mishahara. Tatizo hili mara nyingi huwa linaambatana na kuchelewa kulipwa fedha kwa hizo serikali. Mbali na hayo, tukumbuke kwamba haya yote yalifanyika kwa sababu ya kusawazisha na sababu ya kuweza kuinua na kuendelesha uchumi. Hili linapopatikana huwa ni jambo la kusikitisha sana. Utapata kwamba, kama nilivyosema, wafanyikazi wanateseka. Utapata mtu amefanya kazi yake, ambayo labda pengine amepewa na hizo kaunti na pengine amechukua mkopo katika benki kwa sababu ya kufanya kazi yake. Lakini pesa hizo anaweza kuzipata baada ya mwaka moja au miaka miwili. Kutokana na hayo, ni vyema Bunge hili na Bunge la Seneti, na hata wale wajumbe ambao wako kule kaunti, kuhakikisha kwamba muongozo huu na mwelekeo huu unaendeshwa kwa namna unavyotakikana na kwa namna Wakenya wanafurahia. Vilevile, ningependa kuchukua fursa hii kuiambia Serikali ya Kitaifa kuhakikisha kwamba kuchelewesha fedha ambazo zinapangiwa serikali za kaunti hakupo. Yanapotokea hayo, ndipo yale matatizo yote ambayo tunayoyazungumzia hapa yanatokea. Wengi wameweza kuyazungumzia. Utapata kwamba uchafu umedorora katika kaunti na huduma nyingi hasipo. Hivi sasa, kama sijakosea, kaunti zimepeana ilani kwamba ifikapo tarehe ishirini na nne mwezi huu, basi watasitisha huduma zao zote. Hii ni kwa sababu Serikali ya kitaifa bado haijawapelekea ule mgao wao ambao ulikuwa upelekwe katika ile Bajeti ya mwaka 2020 na 2021. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kweli kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha kwamba Wakenya wamefurahia huduma ambazo zinapatikana katika serikali zote mbili. Wale wanaoongoza katika serikali hizi mbili wahakikishe kwamba Wakenya wameweza kufurahia huduma hizo, wameweza kuwajibika na kazi zao na wameweza kuonyesha uongozi mzuri. Haitakuwa jambo la busara tusimame hapa leo tuanze kulaumiana kwa sababu dunia hii hakuna ambaye ni mkamilifu. Mkamilifu ni Mwenyezi Mungu peke yake. Unapochukua majukumu na kuchukua kiapo cha kuhakikisha kwamba umekubali kuchukua yadhifa unaopewa kama kiongozi, basi ni jambo la busara kuhakikisha kwamba umeweza kutekeleza yale ambayo ni ya usawa. Matatizo ni mengi ambayo yako katika serikali hizi za kaunti. Ukweli ni kwamba kuna dharura na kunahitajika pakubwa kuweza kuyarekebisha matatizo hayo, tukianza na kuhakikisha kwamba migao hii ambayo inagawanywa kila mwaka kwa serikali hizi za kaunti imeweza kufikishwa katika kila kaunti kwa wakati unaofaa bila ya kucheleweshwa. Vile vile, wale wahusika ambao wanasimamia fedha hizi katika sehemu hizo wahakikishe kwamba wameweza kutekeleza zile huduma zinazohitajika kwa namna inayofaa na namna inayotakikana. Vile vile, swala nzima la siasa katika sehemu hizi utapata kwamba kuna malalamishi pia katika kaunti nyingi. Utapata kwamba wale ambao ni wahusika wakuu zaidi wanatembea kisiasa badala ya kutembea kiuongozi. Ninavyofahamu ni kwamba yeyote ambaye ametoka katika kaunti The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}