GET /api/v0.1/hansard/entries/1078382/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1078382,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1078382/?format=api",
"text_counter": 506,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ya kuzungumzia mjadala huu ambao unahusu sheria ya ugavi wa pesa kwa maeneo 47 ya ugatuzi. Ukweli ni kuwa Wakenya walifurahia sana jambo hili la ugatuzi. Lakini vile muda unavyoenda, ikawa kuwa kwanza, pesa zikifika zinafujwa. Pili, pesa hazifiki kwa wakati unaofaa. Tatu, mara nyingine wanavuka mwaka na pesa zote hazijafika kwenye maeneo ya ugatuzi. Wenzangu wamezungumzia masuala ya wanakandarasi ambao wanadai serikali za ugatuzi kila mahali hapa nchini. Hata Serikali kuu pia inadaiwa kulingana na utendajikazi wa wanakandarasi na pesa kuchelewa kuwafikia. Kilio kipo kila mahali. Kilio kikubwa ni kile cha wafanyikazi wa maeneo ya ugatuzi karibu kila mahali. Wanalia kuwa mishahara haijalipwa kwa muda mrefu. Hawa ni Wakenya ambao walikuwa wamesherehekea jambo hili la ugatuzi na sasa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}