GET /api/v0.1/hansard/entries/1078383/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1078383,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1078383/?format=api",
"text_counter": 507,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "ni kama linawaangamiza. Mtu atalipa vipi nyumba pale anapokodisha? Atanunulia watoto wake chakula namna gani? Atasomesha watoto namna gani? Kule tunakotoka katika maeneo bunge ni vilio, vilio, vilio. Hakuna haja ya sisi kuzungumzia suala hili na kuliweka kwenye sheria kwa sababu ugavi wa pesa uko ndani ya sheria. Tutaipitisha sheria hii lakini pesa hazitawafikia wananchi katika maeneo ya ugatuzi. Langu ni kuzungumzia Waziri ambaye anasimamia masuala ya fedha kwenye Serikali ya Kitaifa, Ukur Yatani. Alikuwa gavana kabla hajafika hapo alipo sasa. Anajua matatizo yaliyoko katika maeneo ya ugatuzi. Si hivyo tu. Ukiangalia hata huduma ambazo tunazihitaji katika maeneo ya ugatuzi, wananchi wanateseka kwa sababu hata huduma za afya, maji ya kunywa na kazi za kilimo zimeharibika. Bila wafanyikazi wa Serikali kusaidia wakulima ama wananchi kupata maji ya kunywa, magonjwa yatazidi kila siku kwa sababu utakosa chakula na maji ya kutumia na mwisho itakuwa ni ugonjwa. Huduma za afya kule mashinani zina matatizo makubwa sana kwa sababu fedha hazipo. Utakuta kazi za kandarasi zimefanywa na kuachwa nusu nusu. Wale waliomalizia wameondoka na funguo za maeneo yale. Kwa hivyo, maeneo yale hata hayawezi kutumika. Majengo yamejengwa na yamebaki hayawezi kutumika kwa sababu wanakandarasi hawajalipwa. Hatuwezi kuwa na nchi ambayo tunajivunia kuendelea kama watu wetu wanalia hawapati mishahara. Hatuwezi kuwa na maendeleo kama wananchi hawawezi kupata maji safi ya kunywa. Hatuwezi kusema kuwa tunategemea kilimo nchini wakati wafanyikazi wanaosimamia na kufunza wakulima juu ya kilimo hawajapatiwa mishahara yao kwa miezi hiyo yote."
}