GET /api/v0.1/hansard/entries/1078443/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1078443,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1078443/?format=api",
    "text_counter": 567,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa nafasi hii ya kuchangia Mswada kuhusu fedha zitakazopewa serikali za kaunti katika mwaka wa 2021/2022. Mwanzo, naunga mkono Mswada huu kwa sababu pesa sahihi zinakwenda mashinani tangu tupitishe Katiba mpya mwaka wa 2010. Ninasema hivyo kwa sababu sa hii Wapwani hatuna haja tena ya kusema kuwa Pwani si Kenya. Sa hii tunapata mabillioni ya pesa kila mwaka na tunachagua viongozi miongoni mwetu ambao wanasimamia miradi muhimu ya msingi. Hatuna haja tena ya kumngoja Mtukufu Rais aje mashinani ili tumuombe vitu vidogo vidogo kama miradi ya maji, shule za chekechea na pia hospitali ama dispensary . Kwa hilo, Wakenya siku zote watakuwa wanamshukuru Mheshimiwa Raila Amolo Odinga kwa kuja na Hoja hii ya kubadilisha Katiba. Tumekuwa na magavana kwa miaka minane au tisa hivi. Naomba sana watupee imani zaidi na kuonyesha wananchi na Wakenya wote umuhimu wa fedha hizi. Kwa kweli, Wakenya na viongozi wengi, kama walivyosema hapa Bungeni hivi leo, hawajaona faida au kazi kubwa ambayo fedha hizo zinaweza kufanya kuondoa umaskini katika kaunti zetu. Mumeskia pia baadhi ya viongozi wakisema kuwa pesa za Hazina ya Ustawi wa Maeneo Bunge ya Serikali ya Kitaifa ambazo ni Ksh100 milioni tu na pesa za akina mama za National Government Affirmative ActionFund (NGAAF) wakati mwingine zinasikika zaidi kati ya wananchi kuliko senti za magavana ambazo ni mabilioni. Tunasihi magavana watumie pesa vizuri na waweke mikakati ya kushinda ufisadi katika serikali za kaunti. Hata kama tunatetea waongezewe pesa mwaka huu, waongezewe kupitia miswada kama vile BBI ambayo inataka kuongeza fedha za serikali za kaunti. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}