GET /api/v0.1/hansard/entries/1078446/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1078446,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1078446/?format=api",
"text_counter": 570,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "za kitambo zilikuwa zinakusanya fedha zaidi kuliko serikali za kaunti ilhali serikali za kaunti zina nguvu na mamlaka zaidi kuliko kamati za councils za hapo awali kabla hatujabadilisha Katiba. Wawe wabunifu na waangalie mifano ya magavana wengine humu humu Kenya ambao wametengeneza mitambo ambayo imeongeza thamani ya bidhaa zao, kwa mfano, maembe, maziwa na kadhalika. Bidhaa na mimea za wananchi katika hizo kaunti zimepata soko na zimeleta bei nzuri. Hiyo imeweka pesa nzuri katika mifuko ya wananchi ili waweze kujikimu kimaisha na gharama zao ndogo ndogo za maisha. Viwanda pia vinazalisha kazi. Tunajua ajira ni changamoto kubwa sana nchini mwetu na viwanda hivyo ni njia ya kuzalisha kazi. Iwapo serikali za kaunti na viongozi wao magavana watakuwa wabunifu, basi hata Serikali Kuu ikichelewa kutuma senti, watakuwa na senti za kutumia. Naskia pia pengine hakuna mikakati mizuri. Kuna ufisadi ndani ya pesa zinazokusanywa na hakuna mikakati mizuri ambayo imewekwa. Kwa hivyo, tunahitaji kuweka mikakati mizuri. Tunaomba Senate ifanye hivyo ili kuwe na uhakika kuwa zile pesa zinazokusanywa zinafanyiwa hesabu, zinatambulika na haziendi kwenye mifuko ya watu binafsi. Ningependa kuomba Serikali Kuu vile vile. Hata kama tunahimiza magavana wajitahidi katika kusimamia uchumi na fedha za serikali za kaunti vizuri, serikali hizo ziweze kupata pesa kwa wakati na iwe hakuna muda ambapo senti hizo hazipo. Kuwe hakuna sababu ya wale wanaofanya biashara na kaunti kukosa pesa. Ni jambo la kusikitisha. Inaonekana kuwa watu wana tabia mbaya ya ubinafsi ya kutolipa madeni wakienda uongozini, hata kama kuna fedha za umma. Hawana hiyo tabia ya kulipa. Ni muhimu kwa mteja mkubwa sana kama Serikali kulipa madeni ya wale wanaofanya biashara nao kwa muda. Bila hivyo, tunaharibu uchumi wa nchi. Kuna watu wamechukua mikopo na wameharibikiwa maisha yao kwa sababu ya kuchelewa kulipwa kwa fedha zao, wengine kwa miaka mingi zaidi. Hilo ni jambo litapewa kipao mbele kabla mwaka huu wa kifedha uishe. Walipwe madeni yao ili pesa zianze kuzunguka katika uchumi wetu na kupunguza baadhi ya shida ambazo zimetukumba sana hususan changamoto ya Coronavirus. Tumepata bahati kubwa kuwa na ugatuzi. Nchi zingine jirani zinatamani kuwa na ugatuzi ili wananchi katika sehemu za mashinani waweze kujiamulia miradi yao. Nasikitika kusema kwamba kuna baadhi ya magavana wanadanganya wananchi. Sasa tunaelekea siku ya kupiga kura mwaka wa 2022. Kuna magavana ambao wanazunguka mashinani. Wanafedha nyingi sana za kuzunguka kila sehemu ya kaunti. Wanaambia wananchi kuwa wasipochagua fulani kama gavana, hawatapata basari ambao ni uongo. Ni jukumu la gavana kuhakikisha kuwa uchumi umekuzwa na wananchi wanapesa mfukoni. Ukweli ni kuwa basari za viongozi wote haziwezi kusomesha watoto wote. Muhimu ni uchumi uweze kukuzwa, ili wananchi wapate fedha ya kulipa karo ya watoto wao. Basari zimewekwa pale kwa sababu ya wale walala hoi katika jamii lakini sio za kupewa kila mtu."
}