GET /api/v0.1/hansard/entries/1078447/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1078447,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1078447/?format=api",
"text_counter": 571,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Kwa hivyo, magavana wawache hii tabia ya kudanganya wananchi kuhusu majukumu yao na vile serikali inavyofanya na kuzidi kuwatatiza. Pia, nawasihi magavana mwaka huu na miaka ijayo wawekeze zaidi kwa vile vitu ambavyo ni muhimu kwa wananchi kama maji. Wamepewa jukumu hili. Mvua imechelewa hivi sasa. Kuna sehemu nchini ambapo watu wanakunywa maji ya chumvi. Unasikia hadithi kuwa watoto wanakunywa maji ya chumvi mpaka wanatapika, kwa sababu hakuna maji masafi. Tumekuwa na ugatuzi karibu miaka kumi. Hili ni jambo la kusikitisha. Magavana wanasikia habari hizi lakini hawapeleki maji ya kusaidia kwa dharura. Wamekaa tu kimya wananchi wakipata taabu na hilo ni jukumu lao. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}