GET /api/v0.1/hansard/entries/1078448/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1078448,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1078448/?format=api",
"text_counter": 572,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Magavana wawekeze katika masuala ya afya kwa sababu mengi yamegatuliwa. Hakuna dawa katika hospitali. Madaktari hawatoshi. Shida ya magavana wengi ni kujenga zahanati na hospitali kila pembe za kaunti. Wanaongeza zahanati lakini zile ambazo ziko hazina dawa na madaktari wa kutosha. Nashangaa kwa nini wanataka kuweka mijengo mingi bila kupeana huduma katika sehemu hizo."
}