GET /api/v0.1/hansard/entries/1079485/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1079485,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1079485/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Malengo ya Mswada huu ni kuongeza mapato ya Serikali. Mapato ni muhimu kwa sababu kuna mambo mengi ya kufanywa. Kwa hivyo, mambo haya hayatafanyika isipokuwa waongeze mapato. Nimefurahishwa zaidi na pale kwa wanakandarasi wadogo ambao si Wakenya wafaa kulipa ushuru. Hii ni kwa maana imekuwa kawaida wanakuja wanafanya kazi Kenya, wanachukua pesa zetu na kwenda nayo bila kulipa ushuru. Kwa hivyo, pale nimefurahishwa. Nataka pia niseme kidogo upande wa mafuta. Mafuta yakiongezeka bei, inaongeza gharama zingine za matibabu kwa sababu Wakenya wengi wanabidi kutumia kuni au makaa ambapo moshi unaoingia kina mama unawaathiri mapafu wanakuwa na ugonjwa wa mapafu. Kwa hivyo, vile vile Serikali pia inawajibika kutumia pesa nyingi zaidi katika afya. Sina mengi, naunga mkono. Asante."
}