GET /api/v0.1/hansard/entries/1079836/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1079836,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1079836/?format=api",
"text_counter": 294,
"type": "speech",
"speaker_name": "Endebess, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Robert Pukose",
"speaker": {
"id": 1458,
"legal_name": "Robert Pukose",
"slug": "robert-pukose"
},
"content": " Nashukuru, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa kuchangia hii Bill ya mambo ya finance ambayo ni muhimu ya kukusanya ushuru ili kuweza kuchangia katika Bajeti yetu ya Mwaka 2021/2022. Kwanza, nashukuru Kamati ikiongozwa na Mhe. (Bi) Gladys Wanga kwa kazi nzuri ambayo imefanya. Jambo ambalo nimeona la kushukuru na ambalo tutaliunga mkono ni mambo ya kuongeza ushuru kwa mambo ya pikipiki; kwa watu wa boda boda. Waziri wa NationalTreasury katika Bajeti yake alipanga kuongeza ushuru kwa mambo ya pikipiki kwa asilimia 15. Kamati imeangalia na sisi kama Wabunge tunaiunga Kamati mkono kwamba huo ushuru utolewe kwa mambo ya pikipiki ili watu wa bodaboda waweze kufanya kazi yao kwa njia nzuri. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kama ujuavyo, saa hiii tukiwa katika msimu huu wa Coronavirus, watu wengi wanafanya biashara ya boda boda. Ukiangalia, kwa mfano, juzi jumamosi katika eneo Bunge langu la Endebess, vijana wa boda boda walikuja kwangu wakasema, “Mhe. saa hii vile lockdown imewekwa, sisi kulipia pikipiki ni vigurmu. Unajua wengi wanachukua boda boda kwa deni ili wanaposafirisha watu, wanatengeneza pesa ili waweze kulipia. Kwa sasa, kulipia hizo pikipiki ni shida. Ikiwa tutaongeza ushuru wa asilimia kumi na tano, tutafanya biashara ya boda boda kuwa ngumu sana. Hawa ni watu ambao mapato yao ni ya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}