GET /api/v0.1/hansard/entries/1079839/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1079839,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1079839/?format=api",
    "text_counter": 297,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Endebess, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Robert Pukose",
    "speaker": {
        "id": 1458,
        "legal_name": "Robert Pukose",
        "slug": "robert-pukose"
    },
    "content": "Nafikiri Waswahili wataitafsiri vizuri kusema tuchunge mazingira yetu. Ili tuchunge mazingira yetu, inapaswa tupike chakula kupitia LPG gas. Bei ya mafuta taa imeenda juu kwa sababu ya ile tabia ya watu kuchanganya mafuta taa na petroli. Kwa hivyo, the Ministry ilisema kuwa ni lazima tuweke ushuru wa juu kwa mafuta taa ili wanabiashara wasichanganye na kudhuru magari yetu na kutuletea hasara. Tunapohimiza wananchi watumie LPG gas kwa kupika, inapaswa tuangalie kuwa ushuru wa LPG gas, especially VAT ambayo imewekwa, ifanyiwe zero-rating kama tulivyofanya kwa mkate. Serikali ilitaka kuongeza ushuru kwa mkate. Kamati iliangalia hiyo na kusema hapana. Ushuru uliowekwa kwa mkate si sawa kwa sababu mkate ni food security . Ni chakula ambacho kinaliwa na watu wengi. Kwa hivyo, Kamati ilisema ushuru kwa mkate utolewe. Mimi na wengine hapa Bunge tunaiunga mkono Kamati kwa sababu wameangalia kuwa wananchi wa kawaida wanakula mkate, especially katika institutions nyingi na familia. Mkate ni chakula. Kwa hivyo, tusiweke ushuru kwa chakula kwa sababu tunapofanya hivyo, tunaumiza Mkenya wa kawaida. Kwa hayo mengi, nashukuru na kuunga mkono Kamati katika marekebisho ambayo wataleta ili kuhakikisha kuwa mtu wa kawaida anapata afueni, hasa katika bajeti ya mwaka huu. Naunga mkono Mswada huu."
}