GET /api/v0.1/hansard/entries/1081830/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1081830,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1081830/?format=api",
"text_counter": 321,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Mwanzo, ningependa kupongeza Wizara kwa kufanya majukumu yake. Baada ya wale wanaosaidia kujitoa, walichukua jukumu hilo, wakasimama na wakaanza kurekebisha na kufanya mambo wenyewe. Tumekuwa tukitegemea wafadhili kwa muda mrefu. Ghafla, wafadhili walijitoa. Walijizatiti kusimamia hali ile ngumu ambayo ilikuwa. Damu ni muhimu sana. Naomba wenzangu wapitishe Mswada huu kwa umoja. Wenzangu waliotangulia walisema kwamba hivi vituo vya damu vinafaa kuwa katika kila eneo bunge. Lakini, ziko kwa mikoa sasa. Tukisema ziwe kwa kaunti, hatusemi tuwapatie. Ndio, ziwe za Serikali Kuu lakini ziwe katika kila kaunti kwa sababu kuna kaunti zingine zilizoko mbali na inakuwa ngumu kupata huduma hizi. Damu ni muhimu kwa kila binadamu. Kwa mfano, kama Lamu, kituo cha damu chetu kiko Mombasa. Gharama za usafiri ni nyingi zaidi. Kuweka kituo kule itakuwa ni rahisi. Kwa hivyo, hatusemi zipewe kaunti bali zisimamiwe na Serikali Kuu lakini ziwe katika kila kaunti kwa sababu kwa muda mrefu imekuwa ni kwa kila mkoa. Twapaswa tusonge mbele angalau sasa iwe ni kwa kila kaunti kisha baadaye tuendelee iwe katika kila eneo bunge. Kwa hivyo, bodi inafaa kuhakikisha kuwa hayo mambo mengine yamefanyika. Tunatakiwa kuona maendeleo sio kila mwaka tupo pale pale tulipokuwa."
}