GET /api/v0.1/hansard/entries/1081900/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1081900,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1081900/?format=api",
"text_counter": 41,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Ahsante Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi hii ya kusema katika hilo Ombi. Ombi hili ni muhimu na naliunga mkono. Kwa hakika, watu wengi wanapata shida pande zote za Kenya. Lamu sisi ndio tuna shida zaidi. Kuna hiyo park ambayo iko hapo lakini haitusaidii bali hutuumiza. Afadhali sehemu zingine kama Maasai Mara angalau wanasaidika kwa upande mwingine. Sisi kwetu katika pesa ambazo zimetolewa za malipo, zaidi ya miaka kumi saa hii, zimetolewa milioni sita peke yake na kuna watu wengi wameathirika na wanyama. Kisha wanatuumiza zaidi. Sisi ni watu wa bahari. Wanyama karibu wote wa bahari waliwatoa kwenye orodha ya malipo. Ukienda ukifika baharini ukipigwa na mnyama anayeitwa yeda, haulipwi. Ukipatikana na papa, hulipwi. Na kule tuna wanyama msituni na wanyama baharini. Na saa zingine wanaenda baharini na wanapata hata mamba ndani ya bahari kwa sababu wako karibu na maji ya mto. Kwa hivyo, sisi tuna shida nyingi. Lakini huyu Waziri naye anatoka Coast huko lakini hata sijui ni kwa nini huko Lamu amekusahau. Sijui ni kwa sababu vile kuko mbali. Watu wanalipwa na ikibakia kidogo ndio inarushwa Lamu. Nataka Waziri Balala ajue kwamba Lamu ni Kenya na Lamu ni Pwani. Ahsante, Bw. Spika."
}