GET /api/v0.1/hansard/entries/1083436/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1083436,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1083436/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Mhe. Spika, nilijaribu kwa muda kupata jicho lako. Nataka kujulisha Jumba hili ya kwamba tarehe 8 Juni, nilileta ardhilhali kuhusu wachuuzi ambao wako katika eneo la Mama Ngina Drive. Kumetokea matokeo kadhaa. Ni muhimu kupata mwelekeo wako. Kamati iliyopelekewa ni ya Idara ya Uchukuzi lakini Kamata inayohusika na utalii waliwasiliana na Wizara ya Utalii na Wizara ikafungua rasmi lakini ufunguzi wake sio vile unavyotakikana. Nahofia isije ikaonekana tumeridhika kwa vile imefunguliwa lakini kiasi. Masuali yalioko bado yanaleta kero kwa sababu huwezi kufungulia watu kwa ubaguzi, wengine wanakubaliwa kufanya biashara lakini mwenye ushanga ama mwenye biashara ndogo ndogo hakubaliwi. Mhe. Spika tupatia mwelekeo kama kinara wetu. Njia mwafaka itakuwa ipi ili watu wetu wa Mombasa ambao wameumia tayari kila mmoja wao, licha ya hali yoyote bila ubaguzi, waendelee na biashara zao?"
}