GET /api/v0.1/hansard/entries/1083558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1083558,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1083558/?format=api",
    "text_counter": 263,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "wamesema kuwa bado wanaweza kupata watoto ikiwa watatumia njia hii ya kiteknolojia ambayo inatumiwa pia sehemu zingine ulimwenguni. Kuna maswala tofauti katika huu Mswada ambayo ningependa yaweze kuondolewa wakati tutakuja kwenye Kamati kumaliza kazi ya Mswada huu. Mwanzo, nataka kutaja sehemu ya Katiba ya mwanzo kabisa, sentensi ya kwanza ya Katiba yetu inayosema kuwa Wakenya tunatambua ukubwa wa Mwenyezi Mungu na muumba wa viumbe vyote. Pia kuna sentensi nyingine hapo mwanzoni, ya tano nadhani, ambayo inasema kuwa kama Wakenya tumesema kuwa tutakuza na tutalinda hali ya afya ya sisi kama watu binafsi, jamii na nchi kwa jumla. Kitu cha kwanza ambacho ningependa kisiwe ndani ya sheria hii ni neno katika Mswada huo ambalo linaitwa kwa Kiingereza “ donor ” ama yule mwanamke ambaye atapeana yai lake ama mwanamume ambaye atapeana mbegu yake. Kenya ni nchi ambayo wengi wetu tunafuata dini. Kuna Waislamu na Wakristo. Tunajua katika malezi yetu kuwa kuna vile tunapenda jamii yetu iwe na tunapenda kuheshimu ndoa kati ya watu wawili, mume na mke, waliokuja pamoja na kuoana. Kwa hivyo, naunga mkono kuwa ndoa iwe tu ya watu wawili ambao wamekuja pamoja, lakini isiwe ya watu ambao wako nje ya ndoa. Tayari katika jamii yetu ni kitu ambacho hatuungi mkono. Mara nyingi, tunalalamika sana kuwa kuna wazazi ambao wanalea watoto peke yao, sana sana wanawake, ambao tunaita single mothers. Ni jambo ambalo Serikali yetu inatafutia suluhu. Kwa hivyo, hii pia itakuwa njia ya kuongeza idadi ya single parents ama mzazi mmoja ijapokuwa ni kitu ambacho hatukipendi kwa sababu ya tabia zetu, malezi yetu na uzoefu wetu. Mengine ni kuwa ile mbegu ambaye baba atatoa inaweza kukaa kwa miaka mingi, hata baada ya yeye kufariki. Mbegu hiyo inaweza kubaki na kutengeneza mtoto. Twawaonea huruma watu ambao hawawezi kupata watoto na ndio maana naunga mkono Mswada huu, ila pia wakati mwingine tufikirie mtoto atakayezaliwa. Je, atahisi vipi kuwa tofauti sana na binadamu wengine? Inawezekana kuwa mzazi wake alikufa miaka mitano iliyopita na baada ya mzazi kufariki, ndio anaanza kuumbwa kutumia teknolojia. Kwa Kiingereza, wanatumia neno “ stigm a”. Hata kama twataka kupata watoto na tuna uchungu, lakini pia tufikirie yule mtoto akishazaliwa maoni yake yatakuwa vipi na pia hatajua mzazi wake. Pengine asijue babake ama mamake ni nani. Kuna huo uwezekano. Nishafuatiliza sana kesi nyingi huko Uingereza ambapo teknolojia hii imetumiwa kwa miaka mingi sana. Utaona watoto walioumbwa na teknolojia hii wakitafuta wazazi wao wakifika miaka 20 au 30. Kuna mwingine ambaye alipata ndugu zake wengi. Mbegu ya babake ilitumiwa kwa watu wengi sana. Akafanya bidii kutafuta ndugu zake wote. Kwa hivyo, ina machungu fulani. Kitu kingine ambacho kinanitia wasiwasi ni Kipengele cha 31 kuhusiana na mwanamke kubeba mtoto ambaye yeye hakuchangia yai na ile mbegu ni ya wazazi wengine, yaani surrogacy . Yeye peke yake ndiye anabeba mtoto. Kuna nchi kadhaa ulimwenguni ambazo zimekataa hiyo kwa sababu tofauti tofauti. Mojawapo ni kuwa licha ya kuwa mwanamke anasaidia watu wengine kupata watoto, hali yake ya akili na fikira itaathirika kwa sababu anabeba mtoto kisha anapeana. Ukibeba mtoto kutoka siku ya kwanza, inakuwa ni kama wataka kumlinda. Unamwona kama ni mtoto wako na una uhusiano naye ilhali baada ya kuzaa, inabidi upeane. Ndio maana unaona nchi chache zinakataa hiyo kwa sababu kuna athari. Ndio amesaidia watu wapate mtoto lakini, je, athari kwa yule aliyebeba ni zipi? Kuna jambo lingine ambalo nahofia. Pengine Mheshimiwa hakuwa na nia hii na nafahamu hivyo maanake niko naye siku nyingi, namsikiza na ni mwalimu wangu kwa mambo mengi ya Bunge. Samahani, sina neno lingine la kutumia isipokuwa hili lakini kwa Kiswahili linaitwa “ushoga”. Kwa Kiingereza ni “ homosexuality” . Hii inaweza kutumiwa kama njia ya kupata mtoto hapa nchini Kenya kwa watu ambao wameamua kuwa wataoana mwanamume kwa mwanamume The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}