GET /api/v0.1/hansard/entries/1083824/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1083824,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1083824/?format=api",
    "text_counter": 181,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "mrefu, kampuni hii imewaajiri kama wafanyikazi wa muda mfupi na sheria za nchi haziruhusu kuweka watu hivyo kwa muda mrefu. Kuna wale ambao wamefanya kazi miaka tisa, kumi, kumi na moja, lakini bado hawajapewa mkataba. Ripoti ya Kamati inaonyesha kuwa bado hawajaandikwa mpaka sasa. Wengi wao wamesimamishwa kazi ghafla bila sababu na badala waandikiwe hiyo mikataba, wameachwa na hawajijui wako wapi. Kuna pendekezo kuhusiana na pesa ambazo wafanyikazi hawa wanadai kampuni. Nilipoleta malalamishi haya, Kamati ya Leba ilizuru eneo hilo na waligundua kuwa wafanyikazi walikuwa wanalipwa chini ya kiwango ambacho Serikali ilikuwa imeweka cha mishahara ya wafanyikazi wao. Walifanya hesabu na ikaonekana kuwa wafanyikazi wanadai kampuni hiyo milioni 3.69 na mpaka leo, fedha hizo hazijalipwa kulingana na Ripoti ya Kamati. Kampuni hiyo inadai kuwa hawajaona hao wafanyikazi lakini ukweli ni kuwa ni watu ambao wanaishi hiyo sehemu na iwapo wangetaka msaada wa kuwapata, wangeomba ofisi kadhaa na wananchi pia wa sehemu hiyo wangewatafuta na bila shaka wangewapata ili wawalipe. Pendekezo la tatu ni juu ya mavazi ya kuwalinda dhidi ya kupata majeraha kazini. Baadhi wamenunuliwa lakini wengi bado. Kamati ya Utekelezaji ilipoenda kule tarebe 7/3/2019, waliona kuwa baadhi ya wafanyikazi walikuwa hawana mavazi hayo. Hakuna vyoo na bado wanatumia shambani. Hakuna usafiri pia. Kampuni yenyewe iko mbali na mishahara yao midogo na usipoenda kazini, basi hakuna kazi. Wanalichukua suala la usafiri kama sababu ya kuachishwa kazi. Hivi sasa, wameachisha wazaliwa wa Kaunti ya Kwale kazi na kuajiri wananchi kutoka Magharibi ya nchi. Wameacha sasa wenyeji bila kazi. Kwa ufupi, sijafurahishwa na Ripoti hii na mapendekezo haya. Ningependa kampuni ilazimishwe zaidi kwa sababu mpaka sasa haijatekeleza lolote na ndio maana wameongezewa siku…"
}