GET /api/v0.1/hansard/entries/1083974/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1083974,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1083974/?format=api",
    "text_counter": 131,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Kama alivyozungumza Sen. Murkomen, tungekuwa sasa tunazungumzia idadi ya Wakenya waliopata chanjo. Rais Biden alipochukua uongozi, aliweka ahadi kwamba kwa muda wa siku 100, atachanja watu 300 milioni. Amehakikisha kwamba watu milioni 300 wamepata chanjo. Hapa kwetu, tunaenda hatua mbili mbele na kurudi hatua tano nyuma. Kwa mfano, tumezungumzia mambo ya kukaa mbali na wenzetu na kuvaa barakoa kwa muda mrefu. Hadi sasa, ukienda mitaani wananchi bado hawako tayari kuvaa barakoa wala kuketi mbali na wenzao."
}