GET /api/v0.1/hansard/entries/1083976/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1083976,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1083976/?format=api",
"text_counter": 133,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Juzi nilisafiri kwenda Zanzibar. Kule hakuna kukaa mbali, kuvaa barakoa wala Virusi vya Korona. Watu wanaishi maisha yao kawaida. Ikiwa Serikali ingeweka mikakati thabiti janga hili halingekuwa nasi na watu wangeishi kama kawaida. Je, ni mikakati gani Serikali imeweka kuhakikisha kwamba wananchi wanalindwa? Kuongezea, huku kusuasua kwa Serikali wakati fedha nyingi zimeletwa kupambana na janga hili, kumesababisha watu kukosa imani na kanuni ambazo wananchi wanapewa ilihali Serikali yenyewe haitekelezi. Kwa mfano, wengi wanaoambiwa wavae barakoa, wakishikwa na polisi, wanatiwa rumande. Inabidi watoe hongo ili watoke. Hakuna hata mmoja wa wale walioiba pesa za kupambana na janga la Virusi vya Korona na Mamlaka ya Kushughulikia Utoaji wa Vifaa vya Matibabu nchini, amefikishwa mahakamani, kushitakiwa na kuhukumiwa kwa swala hili. Kwa hivyo, hatuwezi kuwa na nchi ambayo---"
}