GET /api/v0.1/hansard/entries/1084000/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1084000,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1084000/?format=api",
"text_counter": 157,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, siyo wananchi wote wanaovaa barakoya. Seheme ya mashinani ambako nimetoka, sijawahi kuwaona watu wetu wakivaa barakoya. Watu wanendelea na maisha yao ya kama kawaida. Mimi kama Seneta wao ndiye nilishuka gari langu kama nimevaa barakoya na wao waliniangalia na kushangaa sana. Waliniuliza, “Seneta, leo umefunga pua kabisa. Kuna nini limetokea upande wa Kenya ulikotoka?” Niliwauliza kwani bado wanaishi bila kuvaa barakoya na kukaa mbali, walinijibu kuwa hofu ya janga la COVID-19 haiko upande wao."
}