GET /api/v0.1/hansard/entries/1084179/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1084179,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1084179/?format=api",
"text_counter": 336,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Ukiangalia kwa mfano wakunga wale wanaozalisha akina mama wakati wanajifungua, wale ngariba ambao wanapasha tohara wakati vijana wanatiwa jandoni, wengine sasa wanatoa huduma kwa wenye magonjwa kama vile Saratani, kisukari na magonjwa mengi ambayo ni gharama kubwa kupeleka mgonjwa katika zahanati ama hospitali ya kisasa kuweza kupata huduma kama hii. Ugonjwa kama Saratani kwa mfano, umeingia katika vijiji vyetu na wengi wanapata huduma kwa wale ambao ni wafanyikazi wa jamii. Mswada huu utasaidia pia pakubwa kuweza kupambana na mikurupuko ya maradhi tofauti, kwa mfano mikurupuko ya maradhi kama kipindupindu, bilharzia na mengineo ambayo hutokea vijijini ambayo inabidi wananchi watembee safari ndefu kuweza kupata huduma za afya kutoka kwa zile zahanati ambazo zinajulikana. Mswada huu pia utasaidia kusambaza huduma za afya mpaka vijijini kwa sababu sheria inalenga vituo vya afya vya level ya kwanza yaani Level One Hospitals ; hizi ndizo zinalengwa na Mswada huu. Vile vile, Mswada huu utasaidia pakubwa kupambana na magonjwa sugu kama vile Saratani, Kisukari na Corona, kwa sababu hatua zinaweza kuchukuliwa mapema wakati kumetokea visa vya magonjwa kama haya, ili kusikuwe na mkurupuko na magonjwa yasambae katika sehemu zingine. Uwepo wa sheria hii pia itasaidia kupambana na athari za mihadharati katika vijiji vyetu hususan zile sehemu ambazo mihadharati imeingia sana kwa vijana. Kupata huduma za hospitali, kuwapa dawa waadhiriwa wa mihadharati inakuwa shida. Kwa mfano, kule Mombasa kuna sehemu kama vile Coast General Hospital ambapo wanapea huduma za methadone kwa waadhiriwa wa mihadharati. Huduma kama zile zikifanywa katika hospitali kubwa inaathiri huduma zingine ambazo zinatolewa kwa wagonjwa wa kawaida. Kwa hivyo, ikiwa watapewa huduma hii pale katika kijiji, itakuwa ni rahisi na haitaathiri huduma zingine ambazo zinatolewa katika hospitali kubwa kama hizo. Mswada huu pia utasaidia pakubwa azma ya Serikali ya kuweza kufikisha huduma za afya kwa wote ambalo ni lengo kubwa la Serikali hii. Naona kwamba tunalenga kuangalia huduma za afya katika kijiji ama sehemu za mashinani. Hii itasaidia pakubwa kuhakikisha kwamba watu wote wanapata huduma za afya katika Jamuhuri yetu ya Kenya. Pia itasaidia pakubwa kusongeza huduma za afya mashinani kwa sababu sheria inasema kuwa kutakuwa na muhudumu ( Medical Officer of Health ) daktari ambaye ana maarifa na anaweza kuhudumu katika kijiji ama katika sehemu ile ya chini kabisa ya kutoa huduma hizi. Hii inamaanisha kwamba huduma zitaweza kupatikana mashinani na itakuwa ni rahisi kuweza kuwahudumia wananchi katika eneo zile. Hiyo pia itasaidia kuleta teknolojia karibu na wananchi kwa sababu iwapo zahanati hizi zitakuwa na viparakanishi katika eneo za wananachi, zitasaidia kusambaza huduma za afya kirahisi. Kwa mfano vipimo vya afya kwa njia za sasa zitaweza kufanyika bila ya kuwa na matatizo yoyote. Mswada huu pia utasaidia pakubwa kupunguza gharama za matibabu. Tunaona ya kwamba imekuwa donda sugu kwa wananchi kumudu huduma za matibabu. Lakini"
}