GET /api/v0.1/hansard/entries/1084182/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1084182,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1084182/?format=api",
"text_counter": 339,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, naomba Maseneta wenzangu waunge mkono Mswada huu ili kuhakikisha kuwa tuna sheria ya msingi ambayo itatambua kazi ambazo zimekuwa zikifanywa kutoka jadi. Kama nilivyosema awali, kuna watu kama vile wakunga wa kuzalisha kina mama, ngariba wa kupasha watoto tohara na wale ambao wanahudumia wananchi ambao wameathirika na ugonjwa kama vile ukimwi."
}