GET /api/v0.1/hansard/entries/1084276/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1084276,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1084276/?format=api",
    "text_counter": 33,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Laikipia CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Catherine Waruguru",
    "speaker": {
        "id": 13253,
        "legal_name": "Catherine Wanjiku Waruguru",
        "slug": "catherine-wanjiku-waruguru"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika. Niruhusu pia nitoe pongezi kwa Mhe. Yusuf Hassan, Mbunge wa Kamukunji, kwa sababu ya kufikiria mambo ya Mhe. Wangari Maathai. Sisi kama Bunge, hatutaki hili Bunge la Kitaifa lifanywe kuwa kama kaunti ambayo sitaki kutaja. Kuna watu ambao wanaamka na kufanya mambo bila mipango na kuleta uhasama kati ya jamii. Ni lazima iwekwe wazi kwamba kama hatuna sheria ambayo imetungwa, ni njia gani itatumika na kamati ili kupitisha mambo ambayo yanahusu kuname kitu kutumia jina la mtu—natatizwa na Kiswahili kidogo lakini nitaendelea. Mhe. Spika, Mhe. Wangari Maathai alishafariki. Alifanya kazi ngumu na alifurushwa na Serikali ya marehemu Mzee Daniel Moi. Yule mama alifedheheshwa, alivuliwa nguo, alivuliwa hadi uchi na alifanywa kuwa mtu wa kuchekelewa na jamii. Yule mama hakufa moyo. Niruhusu nitumie hii fursa kuwaambia wanawake tulio ndani ya hili Bunge kuwa safari zetu katika siasa si lazima ziwe ni za shangwe na vigelegele. Tutapigwa na teargas, tutakimbizwa na polisi na tutatolewa nguo. Nauliza wanawake tukae kidete kama Mhe. Wangari Maathai. Niruhusu niseme kwa sababu kuna watu ambao wako na mazoea mabovu. Wakishindwa katika sera ama kufanya kazi, wao hukimbiza wanawake wakitumia polisi na teargas . Mimi nitauliza…"
}