GET /api/v0.1/hansard/entries/1084858/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1084858,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1084858/?format=api",
"text_counter": 615,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ni muhimu sisi kujua kuwa sasa hivi watu wengi wanawekwa kwa kikundi kimoja, kuwa kila mtu akitaka damu ni lazima itafutwe kutoka kwa ndugu zake ama majirani na marafiki wakati mtu ambaye ana cheti cha kuonyesha hivi, atakuwa na afueni kuwa amekuwa akitoa damu. Akifika atapatiwa nafasi ya kupata damu bila ya kuulizwa maswali mengi. Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda, watu wengine wanalipishwa pesa ili damu ipatiwe mgonjwa kwa sababu damu haipo. Hao wenye vyeti ni lazima wapendelewe kidogo. Kama damu ipo na wamekuwa wakitoa damu, ni vizuri. Kwa hivyo, nakubaliana na hilo."
}